Posts

Showing posts with the label hot news

ajira 6, 000 za walimu zatangazwa leo bungeni

Image
Na francis kiwali SERIKALI inatarajia kuajiri walimu 6,000 wa masomo ya hisabati na sayansi kwa ajili ya shule za sekondari ifikapo Juni 30, mwaka huu. Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Kakunda alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kuondoa changamoto katika shule za kata ikiwamo upungufu wa walimu wa hisabati na sayansi. Amesema hadi Desemba mwaka 2017, Serikali ilikuwa imeajiri walimu 200 wa Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari. Aidha, Kakunda amesema serikali haijazuia wananchi kuchangia maendeleo ya shule walichokataza ni kumzuia kumpa adha ya kukosa masomo mwanafunzi ambaye ameshindwa kuchangia michango hiyo. Katika swali la pili la nyongeza, Bobali alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu wananchi kuchangia kwenye chakula ambacho wameona kuwa ndiyo mwarobaini wa ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Lindi. K...

Mafriko ya ua watu 10 dar es salaam

Image
Na francis kiwali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema watu 10 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda amesema. “Tunaendelea kupokea taarifa kwa sababu tunawataalamu wetu katika kila kata,” ameongeza Makonda. Ameeleza kuwa Jeshi la kuzima moto, kitengo cha huduma ya haraka, Jeshi la polisi wanaendelea kupokea taarifa kutoka maeneo mbalimbali. Makonda amewarai wananchi walioko katika maeneo salama ni vyema wakatulia majumbani katika kipindi hiki kwani utabiri wa hali ya hewa unaonyesha mvua zitaendelea Jumatatu na Jumanne. Pia amewatahadharisha wale walioko katika maeneo hatarishi akisema: “Ningewaomba waende maeneo ambayo wanaweza kuwa salama, wakati tunatafuta utaratibu mzima wa namna gani tunaweza kupunguza kero. Hususan Changamoto ya maji kutopita katika mitaro." Vyanzo vya habari mjini Dar es Salaam vimeripoti kuwa usafiri wa mabasi ya mwendokasi umesitishwa kutokana na mafuriko eneo la Jangwani. ...

Nionzima alivyo nusulika na ajali ya gari

Image
Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima amenusurika katika ajali aliyoipata eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam. Niyonzima amepata ajali baada ya gari lake kupiga bonde na kupoteza mwelekeo wakati akirejea nyumbani kwake. Taarifa zinaeleza Niyonzima raia wa Rwanda alikuwa mwenyewe kwenye gari na baada akiwa njiani anarejea nyumbani, akakutana na majanga hayo. Juhudi za kumpata zilifanyika, na Niyonzima aliyetua nchini kuichezea Yanga akitokea APR ya Rwanda na baada ya kumpata alithibitisha kwamba ajali na kusema anamshukuru Mungu kwa kuwa haikuwa ajali kubwa. “Gari lilipoteza mwelekeo wakati nikiwa njiani narejea nyumbani na kuingia kwenye msingi. Bahati nzuri sikuwa katika mwendo mkubwa na kuna mtu alikatiza ghafla, nilipojaribu kumkwepa nikapoteza mwelekeo wakati najitahidi kurudi barabarani, nikapiga bonde gari likanishinda nikaingia msingini. “Haukuwa msingi mrefu, baadaye walikuja watu tukalitoa nikaondoka. Nashukuru sikuumia wala yule mtu sikumgonga hivyo hakuna aliyeumia....