Na Mpiraaa umekwishaaa, dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, Mbeya City 1-1 Yanga Dak ya 98, Mpira unaendelea huku dakika ambazo zimeongezwa zikiwa zimemalizika Dak ya 97, Mpira unarushwa kuelekea langoni mwa Yanga Dak ya 95, Muda si mrefu mpira utamalizika Dak ya 92, Mbeya City wanaamka sasa, wanakwenda langoni mwa Yanga lakini mpira unaokolewa DAKIKA SITA ZIMEONGEZWA Dak ya 90, Gooooooli, Mbeya City wanachomoa, Iddy Naddo anafanya matokeo kuwa 1-1 Dak ya 89, Goli Kiki, mpira unapigwa kwenda Yanga Dak ya 88, Mhilu amedondoka chini, machela imeingizwa ndani ya Uwanja kumbeba Dak ya 86, Cannavaro anapewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mchezaji wa Mbeya City Dak ya 85, Yanga wanapanda na mpira kuelekea langoni mwa City, Chirwa anapoteza na wanaokoa Dak ya 83, Mchezaji Juma Abdul kaumizwa, ni faulo kuelekea Mbeya City Dak ya 83, Mbeya wanapambana wakijaribu kusaka bao la kusawazisha, lakini Yanga wamekuwa imara eneo la ulinzi Dak ya 82, Mbeya City wanapata kona, inap...