MAHAKAMA YA KISUTU YATOA AMRI HANS POPE KUKAMATWA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu imetoa amri ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani hapo kuunganishwa katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili rais wa timu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu'.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.
Amri hiyo imetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya wakili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.
Swai alidai kuwa amewatafuta washitakiwa hao toka machi tatu mwaka huu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani
Comments
Post a Comment