HII NDO KAULI YA BOKO KWA YANGA ASEMA HIVI

Mshambuliaji na Nahodha wa Simba, John Bocco, amesema baada ya kushindwa kupata pointi tatu katika mchezo wao wa juzi Jumamosi mbele ya Lipuli, kwa sasa wanajipanga kikamilifu kuhakikisha wanachukua pointi hizo katika mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.

Bocco alikuwa sehemu ya kiko­si cha Simba ambacho kilibanwa mbavu na Lipuli na kujikuta kikipata sare ya kufungana bao 1-1. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Samora mkoani Iringa.

Kwa sasa Simba mechi yao inayokuja ni dhidi ya wapin­zani wao Yanga ambayo itapigwa Aprili 29, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Lipuli, Bocco alisema: “Tulijitahidi kupambana ili tupate matokeo ya pointi tatu lakini Mungu hakuwa upande wetu na tuka­jikuta tukiambulia tu pointi hii moja.

“Kwa sasa mechi imeisha na tunachokiwaza sasa ni kupata pointi katika mchezo ujao (dhidi ya Yanga) tutapambana kuhak­ikisha kwamba tunaondoka na ushindi katika mchezo huo.”
Hii ni sare ya pili kwa Simba dhidi ya Lipuli msimu huu. Katika mechi ya mzunguko wa kwanza jijini Dar, timu hizo pia zilitoka sare ya bao 1-1.

CHANZO: CHAMPIONI

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA