AJIBU AJAALIWA KUPATA MTOTO WA KIKE AANDIKA HAYA KWA UCHUNGU

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa familia ya Mshambuliaji wake, Ibrahim Ajibu, imejaaliwa kupata mtoto wa kike.

Ajibu alishindwa kusafiri na kikosi cha Yanga kuelekea Algiers, Algeria kwa ajili ya mechi ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger.

Mchezaji huyo amesema kuwa ujauzito wa mkewe umepitia changamoto mbalimbali, jambo lililopelekea hofu kubwa kwake lakini ameeleza kumshukuru Mungu kwa kufanikiwa kujifungua salama.

Mbali na mkewe kupata mtoto, Ajibu amesema kuwa ameumizwa na baadhi ya mashabiki waliomtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu wakimuandama kuwa hajasafiri na timu.

"Nashukuru Mungu ametujaalia kupata mtoto wa kike, hapo kabla nilikuwa na hofu kubwa kwasababu ujauzito wa mke wangu ulikuwa na matatizo makubwa, kuna wakati nilikuwa nina hofu juu ya maisha yake.

"Naumizwa na wanaonishambulia kupitia sms kuwa nimegoma kuichezea timu, sina sababu ya kufanya hivyo maana mpira ni kazi yangu" amesema Ajibu.

Hata hivyo Ajibu hajasita kuwasamehe wote waliomshambulia kwa sms hizo kali pamoja na kumuandama katika mitandao mbalimbali ya kijamii, huku akieleza pengine kama wangesikia mke wake amefariki kwa matatizo ya uzazi, wangesema mengine.

"Nawasamehe kwasababu wangesikia mke wangu amefariki kwa matatizo ya uzazi, nadhani wangesema mengine" amesema Ajibu

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA