CHIRWA NA YONDANI WAIGOMEA YANGA
Mkataba wa beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani na ule wa Obrey Chirwa inamalizika mwishoni mwa msimu na wachezaji hao wamegomea mazungumzo ya mikataba mipya.
Yondani amekuwa mhimili wa safu ya ulinzi ya Yanga msimu huu huku Chirwa akiwa kinara wa mabao, ameifunga Yanga mabao 12 kwenye ligi.
Inaelezwa wawili hao wamegomea mazungumzo ya mikataba mipya hivyo wanaweza kuondoka wakiwa wachezaji huru mwisho wa mwezi huu msimu utakapomalizika kama jitihada zaidi za kuwabakisha hazitafanyika.
Kuna taarifa klabu ya ZESCO United ambayo sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga George Lwandamina inawanyemelea wachezaji hao.
Chirwa pia amekuwa akihusishwa na klabu ya Simba japo mwenye mara kadhaa amekanusha juu ya uwezekano wa kutimkia kwa wapinzani hao wa Yanga.
Yondani na Chirwa ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakusafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda nchini Algeria kuikabili USM Alger kwenye mchezo wa kwanza wa kundi D kombe la shirikisho barani Afrika.
Comments
Post a Comment