HUU NDO UJUMBE WA MO SALAH ALIOUANDIKA MWENYEWE
Baada ya kuenea kwa taarifa zilizoeleza kuwa nyota wa Liverpool na timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah atakosekana katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia huko Russia, mchezaji huyo amesema atakuweko kwenye mashindano hayo.
Salah aliumia sana juzi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool baada ya kuchezewa rafu na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos katika mchezo ambao ulimalizika kwa Madrid kushinda mabao 3-1 na kunyakua ubingwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter pia Facebook, Salah ameandika kuwa ana imani atakuwepo kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inayotaraji kuanza siku kadhaa zilizosalia.
Comments
Post a Comment