SIMBA YASAFIRI NA WACHEZAJI HAWA PAMOJA NA WALE WAPYA WOTE
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba walitarajiwa kuondoka leo na kikosi cha watu 25 kwenda nchini Kenya ambao itafanyika michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.
Michuano hiyo itaanza Juni 3 hadi 10 ikishirikisha timu 8 kutoka Tanzania Bana na Visiwani pamoja na wenyeji Kenya.
Simba inaondoka bila mshambuliaji wake nyota, Emmanuel Okwi, nahoadha wake John Bocco huku ikijumuisha wachezaji wake wawili wapaya.
Marcel Kaheza ambaye amerejea Simba akitoa Majimaji atakuwa mmoja wao, lakini Adam Salamba ataondoka Jumamosi kuungana na Simba.
Mmoja wa wakongwe ambaye anarejea katika kiwango chake, Haruna Niyonzima ni kati ya watu waliojumuishwa katika kikosi hicho kitakachoongozwa na Pierre Lechantre.
Msafara utaongozwa na mkongwe Hamisi Kisiwa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Said Tuli pamoja Msemaji wake, Haji Sunday Manara.
KIKOSI:
1. Aishi Manula
2. Said Mohamed
3. Ally Salim
4. Ally Shomary
5. Paul Bukaba
6. Erasto Nyoni
7. Yusufu Mlipili
8. Mohamed Hussein
9. Jonas Mkude
10. Shomari Kapombe
11. Mzamiru Yassin
12. Marcel Kaheza
13. Moses Kitandu
14. Rashid Juma
15. Said Hamis Ndemla
16. Haruna Niyonzima
17. Shiza Kichuya
18. Mohamed Ibrahim
Bechi la Ufundi:
19. Pierre Lechantre
20. Masoud Djuma
21. Mohamed Aimen
22. Muharam Mohamed
23. Richard Robert
24. Yassin Gembe
25. Hamisi Mtambo
Comments
Post a Comment