SPORTS PESA YAIZAWADIA SIMBA SC KWA KUTWAA UBINGWA
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
SPORTS PESA YAIZAWADIA SIMBA SC
Wadhamini wakuu wa Club yetu ya Simba wameizawadia Shilingi Million 100 Simba Sc kama Zawadi ya Ubingwa Wa VPL pesa hiyo imetokewa Leo hii majira ya asubuhi
Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho jijini Nairobi. Jumla ya wachezaji 20 walioondoka ni Makipa Youthe Rostand na Ramadhani Kabwili, Mabeki ni Hassani Kessy, Haji Mwinyi, Abdalah Shaibu Ninja, Pato Ngon yani na Said Juma Makapu. Viungo ni Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Thaban Kamusoko, Maka Edward, Said Mussa Bakari, Baruani Akilimali, Pius Buswita na Yusuph Mhilu. Washambuliaji ni Ibrahim Ajibu, Yohana Mkomola, Matheo Anthony, Juma Mahadhi na Amis Tambwe. Yanga wataanza kibarua chao dhidi ya Kakamega Home Boys Jumapili ya June 03 2018 huku Kocha wake, Mwinyi Zahera aikielezwa ataungana na kikosi chake nchini humo. Waliobaki nchini ni Juma Abdul, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Andrew Vicent Dante, Gadiel Michael, Geofrey Mwashiuya Emmanuel Martin, Nadir Haroub Canavaro na Benno Kakolanya.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amewataka Yanga kutengua ombi lao ndani ya saa 48 la kutaka wasishiriki michuano ya Kombe la KAGAME inayotarajia kuanza Juni 28 2018 jijini Dar es Salaam. Hatua ya imekuja kufuatia uongozi wa klabu hiyo kutuma barua inayoeleza kuomba kujitoa ili kuwapa wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kuja kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC. Karia amefunguka kwa kuwapa Yanga saa 48 kwa maana ya siku mbili kuanzia leo kutengua kauli hiyo akieleza kuwa hata Gor Mahia ambao wapo kundi moja CAF pamoja na Rayon Sports wamethibitisha kushiriki. Rais huyo ameongea kauli hiyo kwa msisitizo akiamini Yanga wanaweza kubadilisha maamuzi hayo aliyosema hayana mashiko ili kuungana na wenzao Simba ambao wamepangwa kundi moja kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Julai 13. Yanga walituma barua hiyo TFF juzi wakiomba kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa lengo la kuwapa wachezaji nafasi kujiandaa katika michuano...
Upangaji wa ratiba na makundi ya Ligi ya Vijana U20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umefanyika leo Alhamis Juni 7,2018 Makao Makuu ya Azamtv. Timu hizo 16 zimepangwa kwenye makundi manne yenye timu nne kila kundi. Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 9,2018 mpaka Juni 21,2018 zikifanyika kwenye Jiji la Dodoma viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM. Kundi A Young Africans Ruvu Shooting Mbeya City Mbao FC Kundi B Simba Singida United Stand United Njombe Mji Kundi C Azam FC Mtibwa Sugar Mwadui FC Majimaji FC Kundi D Tanzania Prisons Lipuli FC Kagera Sugar Ndanda FC Katika kundi A Young Africans watafungua pazia la mashindano hayo dhidi ya Ruvu Shooting saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili Mbeya City dhidi ya Mbao FC Juni 9,2018 saa 10 jioni. Mechi nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya kwanza...
Comments
Post a Comment