YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho jijini Nairobi.

Jumla ya wachezaji  20 walioondoka ni Makipa Youthe Rostand na Ramadhani Kabwili, Mabeki ni Hassani Kessy, Haji Mwinyi, Abdalah Shaibu Ninja, Pato Ngonyani na Said Juma Makapu.


Viungo ni Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Thaban Kamusoko, Maka Edward, Said Mussa Bakari, Baruani Akilimali, Pius Buswita na Yusuph Mhilu.

Washambuliaji ni Ibrahim Ajibu, Yohana Mkomola, Matheo Anthony, Juma Mahadhi na Amis Tambwe.

Yanga wataanza kibarua chao dhidi ya Kakamega Home Boys Jumapili ya June 03 2018 huku Kocha wake, Mwinyi Zahera aikielezwa ataungana na kikosi chake nchini humo.

Waliobaki nchini ni Juma Abdul, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Andrew Vicent Dante, Gadiel Michael, Geofrey Mwashiuya Emmanuel Martin, Nadir Haroub Canavaro na Benno Kakolanya.

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA