Posts

kiwalinews

TSHISHIMBI KUTOKA YANGA KWENDA SIMBA AZUNGUMZA HAYA

Image
Kiungo Papy Tshishimbi ameondoka nchini na kurejea kwao DR Congo kwa ajili ya mapumziko.
Tshishimbi amekuwa akihusishwa na kujiunga na Simba, jambo ambalo limewapa hofu na hasira baadhi ya mashabiki wa Yanga.
Tshishimbi hakuwa amewahi kulizungumzia suala hilo lakini jana amekutana na Salejembe jijini Nairobi, Kenya na kuweka wazi kila kitu.
Tshishimbi amesema anareja kwao kwa mapumziko akiwa bado ni mchezaji wa Yanga na atarejea baada ya mapumziko.
Kuhusiana na suala la Simba, hii ndiyo kauli yake.
“Kuhusu Simba ninasikia tu kwa kweli. Lakini hakuna ambaye amewahi kunifuata tukalizungumzia suala hilo.”
Alipoulizwa kama Simba wakimfuata, yuko tayari kujiunga nao?
“Soka ni biashara rafiki yangu, unajituma na kufanya vizuri ili upae kibiashara na kujiendeleza zaidi. Timu ikifanikiwa, soko linakuwa juu.
“Kama Simba wananihitaji, niko tayari wanaweza kusema wanahitaji nini nami niangalie.”

SIMBA KUWEKA KAMBI ITALY ENDAPO

Image
Imeelezwa kuwa kikosi cha Simba kitasafiri kuweka kambi nchini Italia endapo kitafanikiwa kutwaa ubingwa wa Sportpesa Super Cup nchini Kenya.
Taarifa kutoka ndani kutoka klabu hiyo zimeeleza mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 wataelekea nchini Italia kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Kikosi hicho kesho Jumapili kitakuwa kinashuka Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya kucheza fainali ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia FC.
Simba walitinga hatua huyo baada ya kuwaondosha Kakamega HomeBoyz kutoka Kenya na Gor Mahia wakiiondoa Singida United ya Tanzania.
Fainali ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka la Tanzania na Kenya utaanza majira ya saa 9:00 alasiri

HUYU NDO KOCHA MPYA WA SIMBA ANAE MRITHI PIEERE LECHANTRE

Image
Inaelezwa kuwa mabosi wa klabu ya Simba wameanza mazungumzo na Mfaransa mwingine atakayerithi kiti cha Pierre Lechantre ambaye amenyimwa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Taarifa za ndani zinasema Hubert Velud ni jina la kocha ambaye anahusishwa kuja kuinoa timu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Velud amewahi kuzinoa klabu kubwa barani Afrika ikiwemo Etoile du Sahel, ES Setif, TP Mazembe pia timu ya taifa ya Togo.

Mfaransa huyo anaweza kuja nchini kuchukua nafasi ya Mfaransa mwenzake ambaye mkataba wake umeshamalizika baada ya kusaini miezi 6 inayomalizika siku chache zilizosalia.

Na taarifa zilizopo kwa wekendu hao wa Msimbazi ni kuwa tayari wameshaachana na Lechantre kutokana na kutorodhishwa na kiwango chake ndani ya timu na sasa wameanza mazungumzo na makocha wengine ikiwemo Velud anayehusishwa. 09Jun2018

SIMBA WAACHANA NA LECHANTRE KIIVI

Image
Na Mwandishi Wetu,NAKURU
KOCHA Mfaransa wa Simba SC, Pierre Lechantre na Msaidizi wake, Mtunisia Aymen Hbibi Mohammed wameondoka kwenye kambi ya timu nchini kurejea Dar es Salaam kuunganisha usafiri wa kurudi kwao – maana yake kazi basi.
Simba SC inaendeleza ugonjwa wake wa kutodumu na makocha baada ya kutofautiana na Lechantre aliyeanza kazi Januari 18 tu, mwaka huu.
Lechantre na Aymen Hbibi Mohammed jana walikuwa jukwaani wakati Simba SC ikimenyana Simba SC na Kakamega Homeboyz katika Nusu Fainali ya SportPesa Super Cup na kuibuka na ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Afraha pia.
Timu iliongozwa na Kocha Msaidizi, Mrundi Masoud Juma aliyekaa benchi na kocha wa makipa, Muharami Mohammed ‘Shilton’ na jukwaani alikuwepo Kaimu Rais wa klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’.
Dalili za Simba SC kutodumu na kocha huyo zilianza kuonekana mapema tu baada ya Lechantre kuomba kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon Aprili mwaka huu.
Na baada ya Ligi Kuu kumaliz…

SPORT PESA ITATOA MILLION 250 KWA TIMM ZAKE ENDAPO ITAKIDHI VIGEZO HIVI

Image
Wakati Yanga ikituma barua ya maombi kuelekea TFF ikiomba kujiondoa kwenye mashindano ya KAGAME yanayotaraji kuanza Juni 28 2018, Imeelezwa kuwa SportPesa wameahidi bonazi kwa mshindi wa taji hilo.

Taarifa zimeeleza kuwa mabosi wa kampuni hiyo ya bahati nasibu imeahidi kitita cha bonazi ya shilingi milioni 250 kwa timu ambayo iliyo chini ya udhamini wake endapo itabeba kikombe.

Michuano inayoanza Juni 28 itashirikisha jumla ya timu nne ambazo zipo chini ya udhamini wa SportPesa, timu hizo ni Yanga SC, Simba SC, Gor Mahia FC na AFC Leopards.

Yanga ni miongoni mwa timu hizo lakini endapo kama itashiriki kutokana na kutuma maombi kwenda TFF ikiomba kujiondoa kwa sababu ilizozieleza kuwa inahitaji kuwapa mapumziko wachezaji wake.

Endapo Simba watafanikiwa kutwaa ubingwa wa Kagame watakuwa wamelamba bonazi ya pili baada ya ile milioni 100 waliyochukua kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

Image
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amewataka Yanga kutengua ombi lao ndani ya saa 48 la kutaka wasishiriki michuano ya Kombe la KAGAME inayotarajia kuanza Juni 28 2018 jijini Dar es Salaam.

Hatua ya imekuja kufuatia uongozi wa klabu hiyo kutuma barua inayoeleza kuomba kujitoa ili kuwapa wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kuja kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC.

Karia amefunguka kwa kuwapa Yanga saa 48 kwa maana ya siku mbili kuanzia leo kutengua kauli hiyo akieleza kuwa hata Gor Mahia ambao wapo kundi moja CAF pamoja na Rayon Sports wamethibitisha kushiriki.

Rais huyo ameongea kauli hiyo kwa msisitizo akiamini Yanga wanaweza kubadilisha maamuzi hayo aliyosema hayana mashiko ili kuungana na wenzao Simba ambao wamepangwa kundi moja kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Julai 13.

Yanga walituma barua hiyo TFF juzi wakiomba kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa lengo la kuwapa wachezaji nafasi kujiandaa katika michuano ya CAF amb…