Posts

Showing posts with the label habari

KWA WANA MAKUMIRA WOTE

Image
*_SHUKRANI_ _BAADA YA UCHAGUZI*_  Mimi Gwakisa Mwaipopo &Milembe Vedastus tuliokuwa wagombea wa Urais 2018-2019 wa serikali ya TUMaSO tunapenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kugombea nafasi hii ikiwa ni pamoja na kukamilisha mchakato salama.  Kipekee, tuushukuru uongozi wa chuo, Tume, Serikali ya TUMaSO, na Wabunge wote. Tunashukuru kwa umakini, na uvumilivu wenu.  Aidha, tunapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wana-team wote kwa moyo wa pekee na wa upendo mno. Kwa kweli mm na Milembe hatuna chakuwalipa, Mungu pekee ajua kuwapeni ujira wake.  Tunazidi kuwashukuru mno wanafunzi wenzetu wote wa vitivo vyote kwa kutuunga mkono kwa asilimia 28% ya kura zote. Kwetu tumeona mlivyo-Play your part. Tumeona mlivyo muunga mkono Mhe. Chacha kwa asilimia 32% hakika mmetimiza wajibu wenu wa Kikatiba. Aidha,  tunapenda kuwashukuru mno kwa kumuunga mkono Mhe. Lameck Rais Mteule wa serikali ya TUMaSO kwa kumuunga mkono kwa 38...

HATIMAYE DIAMOND NA ALIKIBA WASHIKANA MIKONO NA KUSALIMIANA LEO MSIBANI KWA AGNES MASOGANGE

Image
Wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba wamekutana katika msiba wa Agnes Masogange na kusalimiana. Mara baada ya wasanii hao kusalimiana kwa kupeana mikono wakiwa katika meza kuu, waombolezaji waliojaa kwenye Viwanja vya Leaders walipiga kelele. Diamond alimsalimia Kiba kwa kumpa mkono, kisha wawili hao walikumbatiana na baada ya tukio hilo, MC Pilipili alisikika akisema: “Unaona sasa, hawana ugomvi hawa.” Kumekuwa na taarifa za wanamuziki hao kuwa na ugomvi kwa muda mrefu ambao hata hivyo, unatajwa kutengenezwa na mashabiki wao wa ‘Team Kiba na Team Diamond.’ Akizungumzia katika viwanja hivyo, Ali Kiba ambaye ametoka kuchukua jiko hivi karibuni, amesema harusi na kifo vyote ni ibada na ndiyo maana amefika kuungana na waombolezaji wengine ingawa bado yupo fungate. Masogange alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge ambako alilazwa kwa siku nne.

Nionzima alivyo nusulika na ajali ya gari

Image
Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima amenusurika katika ajali aliyoipata eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam. Niyonzima amepata ajali baada ya gari lake kupiga bonde na kupoteza mwelekeo wakati akirejea nyumbani kwake. Taarifa zinaeleza Niyonzima raia wa Rwanda alikuwa mwenyewe kwenye gari na baada akiwa njiani anarejea nyumbani, akakutana na majanga hayo. Juhudi za kumpata zilifanyika, na Niyonzima aliyetua nchini kuichezea Yanga akitokea APR ya Rwanda na baada ya kumpata alithibitisha kwamba ajali na kusema anamshukuru Mungu kwa kuwa haikuwa ajali kubwa. “Gari lilipoteza mwelekeo wakati nikiwa njiani narejea nyumbani na kuingia kwenye msingi. Bahati nzuri sikuwa katika mwendo mkubwa na kuna mtu alikatiza ghafla, nilipojaribu kumkwepa nikapoteza mwelekeo wakati najitahidi kurudi barabarani, nikapiga bonde gari likanishinda nikaingia msingini. “Haukuwa msingi mrefu, baadaye walikuja watu tukalitoa nikaondoka. Nashukuru sikuumia wala yule mtu sikumgonga hivyo hakuna aliyeumia....