Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa Msanii Diamond Platnumz, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, ametiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Babu Tale amekamatwa kufuatia amri iliyotolewa Februari 16, 2018 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda Maalum, Wilbard Mashauri iliyoelekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale. Amri hiyo pia, ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine. Hata hivyo, Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama hiyo ikatoa amri nyingine kama hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa wakitafutwa bila mafanikio hadi jana alipokamatwa. Mahakama hiyo iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh250 milioni, baada y...