Posts

Showing posts from April, 2018

MAHAKAMA YA KISUTU YATOA AMRI HANS POPE KUKAMATWA

Image
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu imetoa amri ya Mwenyekiti wa Kamati ya    Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani hapo kuunganishwa katika kesi    ya utakatishaji fedha inayomkabili rais wa timu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu'. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha    kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani. Amri hiyo imetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya wakili    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini    (TAKUKURU), Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao. Swai alidai kuwa amewatafuta washitakiwa hao toka machi tatu mwaka huu    bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani

OKWI NA BOKO WAVUNJA NA KUWEKA REKODI AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA

Image
Wakati kikosi cha Simba kikijiandaa kupambana na Yanga, Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, washambuliaji wa timu hiyo, Mganda, Emmanuel Okwi na John Bocco wamewashangaza wapenzi na mashabiki wa timu hiyo. Imebainika kuwa wachezaji hao wawili wamefanikiwa kuandika rekodi ya pekee ndani ya klabu hiyo ambayo haijawahi kuandikwa na washambuliaji wengine waliowahi kuitumikia timu hiyo kwa zaidi ya miaka sita. Rekodi hiyo ambayo wameiweka wachezaji hao ni ya kufunga mabao mengi mpaka sasa kushinda pacha za washambuliaji wengine waliowahi kuitumikia timu hiyo katika miaka sita iliyopita. Okwi na Bocco wameifungia Simba mabao 33 kati 58 ambayo timu hiyo imeshafunga kwenye ligi kuu msimu huu huku ikiwa na mechi tano mkononi ili kumaliza ligi hiyo. Msimu wa 2011/12, safu ya ushambuliaji ya Simba ilikuwa ikiundwa na Okwi na Mzambia, Felix Sunzu ambapo mpaka mwisho wa msimu walifunga mbao 19 kati 47. Okwi alifunga mabao 12 huku Sunzu akifunga mabao 7. Msimu wa 2012/13, safu ya u

KICHUYA NA MSUVA WAONGELEWA BUNGENI LEO SIKIA YALIYO ZUNGUMZWA

Image
jana katika Makao Makuu ya Bunge jijini Dodoma kwa hoja mbalimbali kuendelea kujadiliwa zinahusiana na masuala ya nchi. Wakati kikao kikielekea mwishoni, Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Wilaya ya Ilala, Mussa Azzan Zungu, aliwamchokea swali la kiaina Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harisson Mwakyembe, kuhusiana na kufungiwa kwa wimbo wa Mwanaume Mashine ulioimbwa na Msanii, Msaga Sumu. Zungu alimuuliza Mwakyembe kwanini ameufungia wimbo huo wakati umewataja wachezaji Simon Msuva (aliyekuwa anaichezea Yanga) na Shiza Kichuya ilihali timu hizo zinakutana kesho kwenye Uwanja wa Taifa. Zungu aliwataja wachezaji hao kutoka na namna mchezo huu wa watani wa jadi jinsi unavyovuta hisia za mashabiki na wadau wengi wa soka nchini ambazo zitakuwa zinavaana Jumapili hii ya Aprili 29 2018. Swali hilo lilipelekea kuwaacha hoi wabunge wengi ambao walianguka kwa kicheki na ndipo Mh. Zungu akafunga kikao na kuwataka wabunge watakutana wakati mwingine kuendelea na vikao

KOCHA WA AZAM FC AFUNGIWA MECHI HIZI KWA KOSA LA KUMTUKANA REFA NA KUAMBIWA HIVI

Image
MZUNGU WA AZAM ASIMAMISHWA LIGI KUU KWA KUMTUSI REFA Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA Mromania wa Azam FC, Aristica Cioba amesimamishwa hadi suala lake la kumtukuna Mwamuzi baada ya mechi kumalizika litakaposikilishwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi kutokana na makosa anayodaiwa kuyafanya katika mechi namba 194 dhidi ya Njombe Mji. Kabla ya kumtukana Mwamuzi, Kocha huyo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) kwa kupinga maamuzi kwa maneno na vitendo katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 15, 2018 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

KOCHA MKONGOMANI WA YANGA ANYANG'ANYWA JEZI YENYE LANGI YA SIMBA AAMBIWA HIVI

Image
Baada ya kuwasili jana mjini Morogoro na kupata nafasi ya kukinoa kikosi cha Yanga kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, jezi ya Kocha Mkongomani Mwinyi Zahera yawa gumzo kwa baadhi ya mashabiki wa timu zote mbili. Zahera alitinga Uwanjani kuishuhudia timu yake mpya akiwa amevalia uzi mweusi wenye micharazo ya rangi nyekundu kwenye mabega, rangi ambayo haijawahi kutumika kabisa katika klabu hiyo yenye maskani yake katika mitaa ya Twiga, iliyo Jangwani, Kariakoo. Baadhi ya mashabiki ikiwemo wale wa Yanga na Simba, wamekuwa wakihoji imekuwa avae rangi ambazo hazitumiki ndani ya klabu. Wapo wale walioandika mitandaoni haswa wa upande wa pili wakitupa vijembe kuwa Mkongo huyo ana damu ya Simba kutokana na rangi hiyo nyekundu. Rangi ya Yanga ambayo inatambulika siku zote ni kijani na njano, pia hivi karibuni wamekuwa wakitumia nyeusi haswa katika mechi za ugenini. Kitendo cha Zahera kuvaa rangi hiyo ambayo hutumiwa na watani zao wa jadi Simba, imekuwa gumzo kubwa zaidi kwa baadhi ya mashabiki

SIMBA WAPEWA ADHABU KALI KWA KOSA HILI HAPA

Image
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita ilipitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao; Mechi namba 200 (Simba 2 vs Tanzania Prisons ). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuwakilishwa na maofisa watatu badala ya wane kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 16, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kitendo chao ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Mechi namba 191 (Simba 3 vs Mbeya City 1).  Klabu ya Simba imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika sita katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 12, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kitendo cha Simba ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo

Download KWANGWALU REMIX BY ERIC OMOND

Image
                    >>>>> download hapa<<<<<

MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA VS YANGA SHUGHULI NZIMA KUANZA SAA MBILI KWA MTINDO HUU

Image
Mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchi kati ya Simba na Yanga Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, unaambiwa shughuli nzima itaanza saa mbili. Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa Uwanja wa Taifa utafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi ili kutoa nafasi kwa watu kuingia. Aidha TFF imesema itaimalisha ulinzi wa nguvu ikiwemo kufungwa kwa Camera zaidi ya 100 ili kurekodi matukio mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika Uwanjani. Mechi hiyo inayowakutanisha watani wa jadi huwa ni ya aina yake na huteka hisia za mashabiki wengi wa timu hizo za Kariakoo. Vikosi vyote vya Simba na Yanga viko mjini Morogoro hivi sasa vikijiandaa na mchezo huo utakaopigwa Jumapili ya wiki hii

WATU SABA WAKAMATWA ARUSHA KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO APRIL 26 KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Image
Watu saba akiwamo mwanamke mmoja wanashikiliwa na Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii. Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amewaambia wanahabari leo Aprili 25 kuwa watu hao wamekamatwa kutokana na sababu za kuhamasisha maandamano Aprili 26 mwaka huu. Ilembo amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakihamasishana kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwamo ya Telegram na WhatsApp. Amesema watu hao wamekamatwa kupitia vitengo vya intelijensia baada ya kuwekewa mitego mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata. Amesema miongoni mwa watuhumiwa hao baadhi yao wapo vyuo vikuu, mitaani na maeneo mengine. Ilembo ameongeza kuwa watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote, huku wakiendelea kuwatafuta wengine kwa njia mbalimbali. "Nasisitiza hakuna maandamano Aprili 26, atakayeandamana atavuna alichopanda kwa kuwa Serikali haijaribiwi," amesema Ilembo

HII NDO KAULI YA BOKO KWA YANGA ASEMA HIVI

Image
Mshambuliaji na Nahodha wa  Simba, John Bocco , amesema baada ya kushindwa kupata pointi tatu katika mchezo wao wa juzi Jumamosi mbele ya  Lipuli , kwa sasa wanajipanga kikamilifu kuhakikisha wanachukua pointi hizo katika mchezo wao ujao dhidi ya  Yanga. Bocco alikuwa sehemu ya kiko­si cha Simba ambacho kilibanwa mbavu na Lipuli na kujikuta kikipata sare ya kufungana bao 1-1. Mechi hiyo ilipigwa  Uwanja wa Samora  mkoani Iringa. Kwa sasa Simba mechi yao inayokuja ni dhidi ya wapin­zani wao  Yanga  ambayo itapigwa Aprili 29, mwaka huu katika  Uwanja wa Taifa jijini Dar. Mara baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Lipuli, Bocco alisema: “Tulijitahidi kupambana ili tupate matokeo ya pointi tatu lakini Mungu hakuwa upande wetu na tuka­jikuta tukiambulia tu pointi hii moja. “Kwa sasa mechi imeisha na tunachokiwaza sasa ni kupata pointi katika mchezo ujao (dhidi ya Yanga) tutapambana kuhak­ikisha kwamba tunaondoka na ushindi katika mchezo huo.” Hii ni sare ya pili kwa

Download new song RAYVANY ft S2KIZZY Pochi Nene

Image
>>>> bofya hapa<<<<

Download wimbo mpya DIAMOND FT JASON DERULA COLOUR

Image
                              >>>> download hapa<<<<<

HATIMAYE DIAMOND NA ALIKIBA WASHIKANA MIKONO NA KUSALIMIANA LEO MSIBANI KWA AGNES MASOGANGE

Image
Wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba wamekutana katika msiba wa Agnes Masogange na kusalimiana. Mara baada ya wasanii hao kusalimiana kwa kupeana mikono wakiwa katika meza kuu, waombolezaji waliojaa kwenye Viwanja vya Leaders walipiga kelele. Diamond alimsalimia Kiba kwa kumpa mkono, kisha wawili hao walikumbatiana na baada ya tukio hilo, MC Pilipili alisikika akisema: “Unaona sasa, hawana ugomvi hawa.” Kumekuwa na taarifa za wanamuziki hao kuwa na ugomvi kwa muda mrefu ambao hata hivyo, unatajwa kutengenezwa na mashabiki wao wa ‘Team Kiba na Team Diamond.’ Akizungumzia katika viwanja hivyo, Ali Kiba ambaye ametoka kuchukua jiko hivi karibuni, amesema harusi na kifo vyote ni ibada na ndiyo maana amefika kuungana na waombolezaji wengine ingawa bado yupo fungate. Masogange alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge ambako alilazwa kwa siku nne.

YANGA YABANWA DAKIKA ZA LALA SALAMA MATOKEO NA MATUKIO YOTE YA MECHI ANGALIA HAPA

Image
Na Mpiraaa umekwishaaa, dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, Mbeya City 1-1 Yanga Dak ya 98, Mpira unaendelea huku dakika ambazo zimeongezwa zikiwa zimemalizika Dak ya 97, Mpira unarushwa kuelekea langoni mwa Yanga Dak ya 95, Muda si mrefu mpira utamalizika Dak ya 92, Mbeya City wanaamka sasa, wanakwenda langoni mwa Yanga lakini mpira unaokolewa DAKIKA SITA ZIMEONGEZWA Dak ya 90, Gooooooli, Mbeya City wanachomoa, Iddy Naddo anafanya matokeo kuwa 1-1 Dak ya 89, Goli Kiki, mpira unapigwa kwenda Yanga Dak ya 88, Mhilu amedondoka chini, machela imeingizwa ndani ya Uwanja kumbeba Dak ya 86, Cannavaro anapewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mchezaji wa Mbeya City Dak ya 85, Yanga wanapanda na mpira kuelekea langoni mwa City, Chirwa anapoteza na wanaokoa Dak ya 83, Mchezaji Juma Abdul kaumizwa, ni faulo kuelekea Mbeya City Dak ya 83, Mbeya wanapambana wakijaribu kusaka bao la kusawazisha, lakini Yanga wamekuwa imara eneo la ulinzi Dak ya 82, Mbeya City wanapata kona, inap

YANGA YAPANGWA NA VIGOGO WA ALGERIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRICA RATIBA IMEKAA HIVI

Image
Droo ya timu zitakazokutana katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika tayari imeshapangwa na Shirikisho la Soka Africa (CAF) ambapo Yanga ipo kundi D lililo na timu za ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Magharibi. Yanga imepangwa kwenye kundi hilo ikiwa na timu za USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda pamoja na Gor Mahia FC ya Kenya. Ratiba inaonesha kuwa Yanga itaanza kucheza na USM Alger ugenini Mei 6 2018, kabla ya kuvaana na Rayon Sports Mei 16 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Baada ya michezo hiyo, Yanga itakuwa mgeni dhidi ya Gor Mahia FC ambapo mechi itapigwa Nairobi Julai 18 2018, kisha baada ya hapo itakuwa mwenyeji dhidi ya Gor Mahia FC tena Julai 29 2018. Ratiba hiyo inaonesha baada ya kukipiga na Gor Mahia, Yanga itawakaribisha USM Alger Uwanja wa Taifa Agosti 19 2018, kisha itasafiri kuelekea Rwanda kukabiliana na Rayon Sports Agosti 29 2018.

KIM JONG _ UN SAYS THERE IS NO NEED FOR FURTHER MISSILE TESTS

Image
Kim Jong-Un says there is no need for further missile tests North Korean leader Kim Jong-un says he has suspended all missile tests and will shut down a nuclear test site. "From 21 April, North Korea will stop nuclear tests and launches of intercontinental ballistic missiles," the country's state news agency said. Mr Kim said further tests were unnecessary because Pyongyang's nuclear capabilities had been "verified". The surprise announcement comes as North Korea prepares for historic talks with South Korea and the US. Mr Kim is due to meet his South Korean counterpart Moon Jae-in next week for the first inter-Korean summit in over a decade, and US President Donald Trump by June. Both countries havebeen pushing Pyongyang to denuclearise and they reacted positively to the latest development. "This is very good news for North Korea and the World - big progress!," Mr Trump tweeted after the announcement. Skip Twitter post by @realDonaldTrump

KIKOSI CHA KWANZA CHA SIMBA DHIDI YA LIPULI LEO 21. 04. 2018

Image
Kikosi cha Simba dhidi ya Lipuli 21 April 2018 1.Aishi Manula 2.Nicolas Gyan 3.Asante Kwasi 4.Juuko Murshid 5.Yusuph Mlipili 6.Erasto Nyoni 7.James Kotei 8.Shomari Kapombe 9.John Bocco 10.Emmanuel Okwi 11. Shiza Kichuya Wachezaji wa Akiba 1.Said Mohammed Nduda 2.Paul Bukaba 3.Mohammed Hussein 4.Juma Luizio 5.Yassin Mzamiru 6.Ndemla Said 7.mAVUGO

Syria returns Legion d'honneur award to France

Image
Syria has returned to France the prestigious Legion d'honneur presented to President Bashar al-Assad, saying he would not wear the award of a country that was a "slave" to America. The move comes days after France said a "disciplinary procedure" for withdrawing the award was under way. France recently joined the US and Britain in bombing Syrian targets over an alleged chemical weapons attack. The award was returned to France via the Romanian embassy in Damascus. President Assad was decorated with the highest class of the award, the Grand Croix, in 2001 after he took power following the death of his father. "The ministry of foreign affairs... has returned to the French republic... the decoration of the Grand Croix of the Legion d'honneur awarded to President Assad," the Syrian foreign ministry said in a statement. "It is no honour for President Assad to wear a decoration attributed by a slave country and follower of the United St