YANGA YAPANGWA NA VIGOGO WA ALGERIA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRICA RATIBA IMEKAA HIVI

Droo ya timu zitakazokutana katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika tayari imeshapangwa na Shirikisho la Soka Africa (CAF) ambapo Yanga ipo kundi D lililo na timu za ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Magharibi.

Yanga imepangwa kwenye kundi hilo ikiwa na timu za USM Alger ya Algeria, Rayon Sports ya Rwanda pamoja na Gor Mahia FC ya Kenya.

Ratiba inaonesha kuwa Yanga itaanza kucheza na USM Alger ugenini Mei 6 2018, kabla ya kuvaana na Rayon Sports Mei 16 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Baada ya michezo hiyo, Yanga itakuwa mgeni dhidi ya Gor Mahia FC ambapo mechi itapigwa Nairobi Julai 18 2018, kisha baada ya hapo itakuwa mwenyeji dhidi ya Gor Mahia FC tena Julai 29 2018.

Ratiba hiyo inaonesha baada ya kukipiga na Gor Mahia, Yanga itawakaribisha USM Alger Uwanja wa Taifa Agosti 19 2018, kisha itasafiri kuelekea Rwanda kukabiliana na Rayon Sports Agosti 29 2018.

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA