Posts

Showing posts from June, 2018

TSHISHIMBI KUTOKA YANGA KWENDA SIMBA AZUNGUMZA HAYA

Image
Kiungo Papy Tshishimbi ameondoka nchini na kurejea kwao DR Congo kwa ajili ya mapumziko. Tshishimbi amekuwa akihusishwa na kujiunga na Simba, jambo ambalo limewapa hofu na hasira baadhi ya mashabiki wa Yanga. Tshishimbi hakuwa amewahi kulizungumzia suala hilo lakini jana amekutana na Salejembe jijini Nairobi, Kenya na kuweka wazi kila kitu. Tshishimbi amesema anareja kwao kwa mapumziko akiwa bado ni mchezaji wa Yanga na atarejea baada ya mapumziko. Kuhusiana na suala la Simba, hii ndiyo kauli yake. “Kuhusu Simba ninasikia tu kwa kweli. Lakini hakuna ambaye amewahi kunifuata tukalizungumzia suala hilo.” Alipoulizwa kama Simba wakimfuata, yuko tayari kujiunga nao? “Soka ni biashara rafiki yangu, unajituma na kufanya vizuri ili upae kibiashara na kujiendeleza zaidi. Timu ikifanikiwa, soko linakuwa juu. “Kama Simba wananihitaji, niko tayari wanaweza kusema wanahitaji nini nami niangalie.”

SIMBA KUWEKA KAMBI ITALY ENDAPO

Image
Imeelezwa kuwa kikosi cha Simba kitasafiri kuweka kambi nchini Italia endapo kitafanikiwa kutwaa ubingwa wa Sportpesa Super Cup nchini Kenya. Taarifa kutoka ndani kutoka klabu hiyo zimeeleza mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 wataelekea nchini Italia kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi. Kikosi hicho kesho Jumapili kitakuwa kinashuka Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya kucheza fainali ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia FC. Simba walitinga hatua huyo baada ya kuwaondosha Kakamega HomeBoyz kutoka Kenya na Gor Mahia wakiiondoa Singida United ya Tanzania. Fainali ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka la Tanzania na Kenya utaanza majira ya saa 9:00 alasiri

HUYU NDO KOCHA MPYA WA SIMBA ANAE MRITHI PIEERE LECHANTRE

Image
Inaelezwa kuwa mabosi wa klabu ya Simba wameanza mazungumzo na Mfaransa mwingine atakayerithi kiti cha Pierre Lechantre ambaye amenyimwa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo. Taarifa za ndani zinasema Hubert Velud ni jina la kocha ambaye anahusishwa kuja kuinoa timu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. Velud amewahi kuzinoa klabu kubwa barani Afrika ikiwemo Etoile du Sahel, ES Setif, TP Mazembe pia timu ya taifa ya Togo. Mfaransa huyo anaweza kuja nchini kuchukua nafasi ya Mfaransa mwenzake ambaye mkataba wake umeshamalizika baada ya kusaini miezi 6 inayomalizika siku chache zilizosalia. Na taarifa zilizopo kwa wekendu hao wa Msimbazi ni kuwa tayari wameshaachana na Lechantre kutokana na kutorodhishwa na kiwango chake ndani ya timu na sasa wameanza mazungumzo na makocha wengine ikiwemo Velud anayehusishwa. 09 Jun 2018

SIMBA WAACHANA NA LECHANTRE KIIVI

Image
Na Mwandishi Wetu,   NAKURU KOCHA Mfaransa wa Simba SC, Pierre Lechantre na Msaidizi wake, Mtunisia Aymen Hbibi Mohammed wameondoka kwenye kambi ya timu nchini kurejea Dar es Salaam kuunganisha usafiri wa kurudi kwao – maana yake kazi basi. Simba SC inaendeleza ugonjwa wake wa kutodumu na makocha baada ya kutofautiana na Lechantre aliyeanza kazi Januari 18 tu, mwaka huu. Lechantre na Aymen Hbibi Mohammed jana walikuwa jukwaani wakati Simba SC ikimenyana Simba SC na Kakamega Homeboyz katika Nusu Fainali ya SportPesa Super Cup na kuibuka na ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Afraha pia. Timu iliongozwa na Kocha Msaidizi, Mrundi Masoud Juma aliyekaa benchi na kocha wa makipa, Muharami Mohammed ‘Shilton’ na jukwaani alikuwepo Kaimu Rais wa klabu, Salim Abdallah ‘Try Again’. Dalili za Simba SC kutodumu na kocha huyo zilianza kuonekana mapema tu baada ya Lechantre kuomba kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon Aprili mwaka huu. Na b

SPORT PESA ITATOA MILLION 250 KWA TIMM ZAKE ENDAPO ITAKIDHI VIGEZO HIVI

Image
Wakati Yanga ikituma barua ya maombi kuelekea TFF ikiomba kujiondoa kwenye mashindano ya KAGAME yanayotaraji kuanza Juni 28 2018, Imeelezwa kuwa SportPesa wameahidi bonazi kwa mshindi wa taji hilo. Taarifa zimeeleza kuwa mabosi wa kampuni hiyo ya bahati nasibu imeahidi kitita cha bonazi ya shilingi milioni 250 kwa timu ambayo iliyo chini ya udhamini wake endapo itabeba kikombe. Michuano inayoanza Juni 28 itashirikisha jumla ya timu nne ambazo zipo chini ya udhamini wa SportPesa, timu hizo ni Yanga SC, Simba SC, Gor Mahia FC na AFC Leopards. Yanga ni miongoni mwa timu hizo lakini endapo kama itashiriki kutokana na kutuma maombi kwenda TFF ikiomba kujiondoa kwa sababu ilizozieleza kuwa inahitaji kuwapa mapumziko wachezaji wake. Endapo Simba watafanikiwa kutwaa ubingwa wa Kagame watakuwa wamelamba bonazi ya pili baada ya ile milioni 100 waliyochukua kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

Image
Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amewataka Yanga kutengua ombi lao ndani ya saa 48 la kutaka wasishiriki michuano ya Kombe la KAGAME inayotarajia kuanza Juni 28 2018 jijini Dar es Salaam. Hatua ya imekuja kufuatia uongozi wa klabu hiyo kutuma barua inayoeleza kuomba kujitoa ili kuwapa wachezaji wake mapumziko kwa ajili ya kuja kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC. Karia amefunguka kwa kuwapa Yanga saa 48 kwa maana ya siku mbili kuanzia leo kutengua kauli hiyo akieleza kuwa hata Gor Mahia ambao wapo kundi moja CAF pamoja na Rayon Sports wamethibitisha kushiriki. Rais huyo ameongea kauli hiyo kwa msisitizo akiamini Yanga wanaweza kubadilisha maamuzi hayo aliyosema hayana mashiko ili kuungana na wenzao Simba ambao wamepangwa kundi moja kushiriki mashindano hayo yatakayomalizika Julai 13. Yanga walituma barua hiyo TFF juzi wakiomba kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa lengo la kuwapa wachezaji nafasi kujiandaa katika michuano

BUNGE LEO LAZUNGUMZA HAYA KUHUSU SIMBA KUFIKA FAINAL SPORT PESA

Image
.                                    BOFA HAPA

YANGA WAJITOA KWENYE MASHINDANO YA KAGAME KISA HIKI HAPA

Image
Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Yanga umewaandikia barua TFF kuwaomba kujitoa katika mashindano ya Kagame CUP yanayotarajiwa kuanza June 28 mpaka Julai 13 2018 jijini Dar es Salaam. Sababu za msinngi zilizofikia Yanga kuandika barua hiyo ni kufanya maandalizi ya michunao ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watacheza na Gor Mahia FC ya Kenya, Julai 18 jijini Nairobi. Kutokana na muingiliano wa ratiba ya KAGAME na CAF, Yanga wameona ni vema kuwapatia wachezaji wao mapumziko ili kuwapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya tatu baada ya kucheza na USM Alger pia Rayon Sports ya Rwanda. Taarifa hizo zinazoelezwa kutoka Yanga kupitia viongozi wa Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo, wameazimia kufanya maamuzi hayo ili kuepuka kubanwa na muingiliano wa ratiba hiyo ambayo imekuwa si rafiki kwao. Kufuatia kuandika barua hiyo ya kuomba kujiondoa, Yanga wanakuwa wameikwepa Simba kwenye mashindano ambapo walikuwa wamepangwa pamoja na mabing

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA

Image
Upangaji wa ratiba na makundi ya Ligi ya Vijana U20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umefanyika leo Alhamis Juni 7,2018 Makao Makuu ya Azamtv. Timu hizo 16 zimepangwa kwenye makundi manne yenye timu nne kila kundi. Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 9,2018 mpaka Juni 21,2018 zikifanyika kwenye Jiji la Dodoma viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM. Kundi A Young Africans  Ruvu Shooting  Mbeya City  Mbao FC  Kundi B Simba  Singida United  Stand United Njombe Mji  Kundi C  Azam FC  Mtibwa Sugar  Mwadui FC  Majimaji FC  Kundi D  Tanzania Prisons  Lipuli FC  Kagera Sugar  Ndanda FC Katika kundi A Young Africans watafungua pazia la mashindano hayo dhidi ya Ruvu Shooting saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili Mbeya City dhidi ya Mbao FC Juni 9,2018 saa 10 jioni. Mechi nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya kwanza ni za kundi C ambapo Azam FC watacheza na Mtibwa Sugar saa 8 mchana ikifuatiwa

MASHABIKI WA YANGA WADAKWA NA POLISI NCHINI KENYA KISA HIKI HAPA

Image
BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA WAKISHUHUDIA BAADHI YA MECHI ZILIZOCHEZWA KWENYE UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM. HAWA SI WALE WALIONASWA MJINI NAKURU. Na Mwandishi Wetu, Nakuru Baadhi ya mashabiki waliosafiri kuja mjini hapa kuishangilia timu yao walijikuta wakiingia mikononi mwa Polisi kwa zaidi ya saa tatu. Mashabiki hao walidakwa nje ya Uwanja wa Afra mji hapa wakiuza tiketi za mechi ya robo fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kati ya Simba dhidi ya Kariobang Sharks. Mambo yalikuwa hivi, siku moja kabla mashabiki hao walifika hapa kuishuhudia Yanga ikicheza na Kakamega Homeboyz. Walipowasili, tayari kipindi cha kwanza kiliisha na Yanga ilishalala kwa mabao 2-1, wakaingia na kushuhudia dakika 45 za mwisho, matokeo yakawa 3-1, Yanga ikiondolewa. Kutokana na hali hiyo, waliona bora kusubiri waone na mechi ya watani wao Simba. Wakapata wazo la kukutana na baadhi ya maofiza wa SportPesa ambao ni wadhamini wa timu yao, wawasaidie tiketi za kuingilia

KAGAME YAZIKUTANISHA SIMBA NA YANGA MAPEEEEMA RATIBA NZIMA HII HAPA

Image
Wakongwe wa soka Tanzania, Simba SC na Yanga SC wamepangwa Kundi C katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13 mwaka huu mjini Dar es Salaam. Akitaja makundi ya michuano hiyo, Katibu wa kudumu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye alisema kwamba pamoja na Simba na Yanga, timu nyingine katika Kundi hilo ni Dakadaha ya Somalia na Saint George ya Ethiopia. Musonye alisema kwamba Kundi A linaundwa na timu za Azam FC, KCCA ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini, wakati Kundi B linaundwa na timu za Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti. Musonye aliishukuru Tanzania kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo na akasema kwamba anatarajia itafana kwa sababu ya rekodi ya nchi hii kuandaa mashindano yaliyokuwa na msisimko mkubwa miaka ya nyuma. Musonye ambaye alisema mashindano yatafanyika viwanja vya Taifa na

ZAWADI NONO HII HAPA KWA WACHEZAJI WA SIMBA ENDAPO WATATWAA UBINGWA SPORT PESA

Image
Hatimaye klabu ya Simba imefunguka na kusema fedha zote za ubingwa wa Sports Pesa Super Cup watapewa wachezaji. Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema fedha zote dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 66) kama watabeba ubingwa zitakuwa mali ya wachezaji. “Tayari tumezungumza nao na kuwaeleza kuhisiana na suala hilo kwamba fedha zote zitaenda kwao,” alisema. Manara amesema hayo mara tu baada ya Simba kushinda kwa mikwaju ya penalti na kutinga nusu fainali. Simba imeing’oa Kariobang Sharks kwa penalti 3-2 baada ya mechi kwisha bila bao katika dakika 90.

YANGA YANASA SAINI YA KIFAA HIKI TOKA BENINI TAYARI KWA SPORT PESA

Image
Wakati vuguvugu la usajili Bongo likiwa linaendelea, tetesi zinaeleza kuwa Yanga imemalizana na Mshambuliaji Mbenin, Marcellin Koukpo, aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Buffles du Burgou nchini kwao. Yanga ambayo usajili wake unaonekana kuwa wa kimyakimya haijaweza kuweka wazi kuhusiana na kumyaka mshambuliaji huyo ambaye inaelezwa amekuja kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliyetimkia Azam FC. Taarifa zinaeleza kuwa Koukpo amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumia mabingwa hao wa historia katika Ligi Kuu Bara kwa kuutwaa mara 27. Imeelezwa pia mchezaji huyo ataungana na kikosi cha Yanga nchini Kenya, tayari kwa michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho

SIMBA YADAKA SAIN YA MSHAMBULIAJI HUYU AINDOKA KWENDA KENYA

Image
Mshambuliaji Mohammed Rashid anatarajia kuanza kuichezea Simba katika michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza keshokutwa mjini Nakuru, Kenya. Mohammed amejiunga na Simba akitokea Prisons na taarifa zinaeleza kwamba amemalizana na Simba jana usiku. “Kweli wamemalizana na yeye sasa ni safari ya kwenda Kenya kwa ajili ya michuano ya SportsPesa,” kilieleza chanzo. Hivi karibuni mshambuliaji huyo alikataa kuongeza mkataba na Prisons ingawa hakuwa amesema anataka kufanya nini. Taarifa zinaeleza alikataa kuongeza mkataba mpya baada ya kukubaliana jambo na Simba, hivyo alikuwa akisubiri kumalizika kwa msimu.

ZIDANE AJIUZURU KUIFUNDISHA MADRID KISA HIKI HAPA

Image
Kocha Zinedine Zidane ametangaza kujizulu kuifundisha soka klabu ya Real Madrid ikiwa ni siku chache baada ya kuipa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya. Zidane ameeleza kuwa kuwa kila kitu kinahitaji mabadiliko hivyo ni wakati wa mtu mwingine kuingoza klabu hiyo yenye historia kubwa katika nchi ya Spain. Kocha huyo amefunguka kwa kusema kuwa amefarijika kuwa mmoja kati ya waliofanikisha Real Madrid kutwaa mataji 13 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuweza kuwa sehemu ya historia hiyo. Kocha huyo amesema Real Madrid inahitaji kuendeleza rekodi yake ya kufanya vizuri haswa kuzidi kupata matokeo katika michuano mbalimbali mikubwa. "Kitu ninachokiwaza ni timu iendelee kupata matokeo, inahitaji kuwa na mabadiliko na inahitaji mtu mwingine, naipenda Real Madrid" amesema Zizou. Zizou anaondoka Madrid akiweka historia ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mara tatu mfululizo na kuweka historia kubwa ndani ya Santiago Bernabeu.