YANGA YANASA SAINI YA KIFAA HIKI TOKA BENINI TAYARI KWA SPORT PESA


Wakati vuguvugu la usajili Bongo likiwa linaendelea, tetesi zinaeleza kuwa Yanga imemalizana na Mshambuliaji Mbenin, Marcellin Koukpo, aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Buffles du Burgou nchini kwao.

Yanga ambayo usajili wake unaonekana kuwa wa kimyakimya haijaweza kuweka wazi kuhusiana na kumyaka mshambuliaji huyo ambaye inaelezwa amekuja kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliyetimkia Azam FC.

Taarifa zinaeleza kuwa Koukpo amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumia mabingwa hao wa historia katika Ligi Kuu Bara kwa kuutwaa mara 27.

Imeelezwa pia mchezaji huyo ataungana na kikosi cha Yanga nchini Kenya, tayari kwa michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA