SIMBA YADAKA SAIN YA MSHAMBULIAJI HUYU AINDOKA KWENDA KENYA



Mshambuliaji Mohammed Rashid anatarajia kuanza kuichezea Simba katika michuano ya SportPesa Super Cup inayoanza keshokutwa mjini Nakuru, Kenya.

Mohammed amejiunga na Simba akitokea Prisons na taarifa zinaeleza kwamba amemalizana na Simba jana usiku.

“Kweli wamemalizana na yeye sasa ni safari ya kwenda Kenya kwa ajili ya michuano ya SportsPesa,” kilieleza chanzo.

Hivi karibuni mshambuliaji huyo alikataa kuongeza mkataba na Prisons ingawa hakuwa amesema anataka kufanya nini.

Taarifa zinaeleza alikataa kuongeza mkataba mpya baada ya kukubaliana jambo na Simba, hivyo alikuwa akisubiri kumalizika kwa msimu.

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA