MASHABIKI WA YANGA WADAKWA NA POLISI NCHINI KENYA KISA HIKI HAPA
BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA WAKISHUHUDIA BAADHI YA MECHI ZILIZOCHEZWA KWENYE UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM. HAWA SI WALE WALIONASWA MJINI NAKURU. |
Na Mwandishi Wetu, Nakuru
Baadhi ya mashabiki waliosafiri kuja mjini hapa kuishangilia timu yao walijikuta wakiingia mikononi mwa Polisi kwa zaidi ya saa tatu.
Mashabiki hao walidakwa nje ya Uwanja wa Afra mji hapa wakiuza tiketi za mechi ya robo fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kati ya Simba dhidi ya Kariobang Sharks.
Mambo yalikuwa hivi, siku moja kabla mashabiki hao walifika hapa kuishuhudia Yanga ikicheza na Kakamega Homeboyz.
Walipowasili, tayari kipindi cha kwanza kiliisha na Yanga ilishalala kwa mabao 2-1, wakaingia na kushuhudia dakika 45 za mwisho, matokeo yakawa 3-1, Yanga ikiondolewa.
Kutokana na hali hiyo, waliona bora kusubiri waone na mechi ya watani wao Simba. Wakapata wazo la kukutana na baadhi ya maofiza wa SportPesa ambao ni wadhamini wa timu yao, wawasaidie tiketi za kuingilia uwanjani.
Maofisa hao wa SportPesa walitekeleza hilo ikiwa ni pamoja na kuwapa fulana. Baadhi yao wakaingia uwanjani na wengine wakabaki wakiziuza na hapo ndipo walipodakwa na Polisi.
Walishikiliwa hadi mechi ilipoisha na taarifa zilielezwa waliachiwa baadaye ingawa walikuwa mbogo baada ya mechi ya Simba ambao walikuwa wamefuzu kwenda nusu fainali ya SportPesa Super Cup.
Simba imeingia hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Kariobang Sharks ya Kenya na sasa inasubiri kuwavaa Kakamega Homeboyz
Comments
Post a Comment