SIMBA KUWEKA KAMBI ITALY ENDAPO
Imeelezwa kuwa kikosi cha Simba kitasafiri kuweka kambi nchini Italia endapo kitafanikiwa kutwaa ubingwa wa Sportpesa Super Cup nchini Kenya.
Taarifa kutoka ndani kutoka klabu hiyo zimeeleza mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 wataelekea nchini Italia kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Kikosi hicho kesho Jumapili kitakuwa kinashuka Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya kucheza fainali ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia FC.
Simba walitinga hatua huyo baada ya kuwaondosha Kakamega HomeBoyz kutoka Kenya na Gor Mahia wakiiondoa Singida United ya Tanzania.
Fainali ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka la Tanzania na Kenya utaanza majira ya saa 9:00 alasiri
Comments
Post a Comment