KWA WANA MAKUMIRA WOTE



*_SHUKRANI_ _BAADA YA UCHAGUZI*_ 

Mimi Gwakisa Mwaipopo &Milembe Vedastus tuliokuwa wagombea wa Urais 2018-2019 wa serikali ya TUMaSO tunapenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kugombea nafasi hii ikiwa ni pamoja na kukamilisha mchakato salama. 

Kipekee, tuushukuru uongozi wa chuo, Tume, Serikali ya TUMaSO, na Wabunge wote. Tunashukuru kwa umakini, na uvumilivu wenu. 

Aidha, tunapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wana-team wote kwa moyo wa pekee na wa upendo mno. Kwa kweli mm na Milembe hatuna chakuwalipa, Mungu pekee ajua kuwapeni ujira wake. 

Tunazidi kuwashukuru mno wanafunzi wenzetu wote wa vitivo vyote kwa kutuunga mkono kwa asilimia 28% ya kura zote. Kwetu tumeona mlivyo-Play your part. Tumeona mlivyo muunga mkono Mhe. Chacha kwa asilimia 32% hakika mmetimiza wajibu wenu wa Kikatiba. Aidha,  tunapenda kuwashukuru mno kwa kumuunga mkono Mhe. Lameck Rais Mteule wa serikali ya TUMaSO kwa kumuunga mkono kwa 38%. Hapa tunapenda kusema, " **Hongera* *Mheshimiwa* *Rais* **Mteule na Makamu wake.* Hongera TUMaSO kwa kupata viongozi awapya wa Awamu ya 10. Nasi tume-Play our part kwa kutimiza haki yetu ya msingi na kuonesha nia ya kuitumikia jamii ikiwa ni pamoja na kuonesha njia wengine kwamba tukiamua kwa dhati *tunaweza* kuwa viongozi bora ktk jamii.

Hata hivyo tunapenda kutumia fursa hii kuwaalika wanafunzi wengine kujitokeza ili kuweza kutumia fursa ya kuwa viongozi ktk jamii yetu bila kujali rangi, kabila, dini, jinsia, au vitivo vyetu. Mm, Chacha, na Lameck na wagombea wenza tumethubutu. Ni wasaa wa wengine kutumia fursa ktk nafasi za ubunge, uwaziri, Uspika n.k bila kuweka mipaka ya vyama, rangi, Ukanda, jinsia na mengine mengi. Jambo la msingi ni *kupima uwezo* wa Mtu ikiwa anaweza kuwa kiongozi mwenye kuifaa jamii. 

All the best Mhe. Mteule Lameck na Makamu! Msiogope, msitetereke wala kuwa na hofu. Mungu aliyewapa nafasi hii atawawezesha kuanza na kumaliza vyema. 

Mwisho ninawiwa binafsi kusema wazi na kwa dhati kwa ajili ya wale wote waliotumia matusi na lugha za kudhalilisha wakisema wanafanya siasa. Siasa sio kuchafua, kudhalilisha wengine bali ni mfumo unaomruhusu mtu kuonesha ukomavu na ueledi wake ktk kuiletea jamii maendeleo yenye tija pasipo kujali Chama,  dini, kabila,  rangi, au elimu yake. *Nimewasamehe** wale wote walionitukana, nidhalilisha na kusambaza habari za uongo kwa nia ya wao kupata kibali kisicho cha kudumu. Kimsingi kwangu chuki ni mzigo mzito sana kuubeba, bali upendo ni mzigo mwepesi mnoo. Kamwe tusikubali kuwa washabiki wanaobomoa maadili na msingi ya jamii yetu, bali wanaoijenga jamii kwa kupima na kujenga hoja.

Mungu ibariki Serikali ya Awamu ya 10, Mungu bariki chuo chetu.  Mungu ibariki Tanzania.🖐🖐

 *Yes we can, Play your part!*

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA