Posts

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

Image
Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho jijini Nairobi. Jumla ya wachezaji  20 walioondoka ni Makipa Youthe Rostand na Ramadhani Kabwili, Mabeki ni Hassani Kessy, Haji Mwinyi, Abdalah Shaibu Ninja, Pato Ngon yani na Said Juma Makapu. Viungo ni Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Thaban Kamusoko, Maka Edward, Said Mussa Bakari, Baruani Akilimali, Pius Buswita na Yusuph Mhilu. Washambuliaji ni Ibrahim Ajibu, Yohana Mkomola, Matheo Anthony, Juma Mahadhi na Amis Tambwe. Yanga wataanza kibarua chao dhidi ya Kakamega Home Boys Jumapili ya June 03 2018 huku Kocha wake, Mwinyi Zahera aikielezwa ataungana na kikosi chake nchini humo. Waliobaki nchini ni Juma Abdul, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Andrew Vicent Dante, Gadiel Michael, Geofrey Mwashiuya Emmanuel Martin, Nadir Haroub Canavaro na Benno Kakolanya.

SIMBA YASAFIRI NA WACHEZAJI HAWA PAMOJA NA WALE WAPYA WOTE

Image
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba walitarajiwa kuondoka leo na kikosi cha watu 25 kwenda nchini Kenya ambao itafanyika michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup. Michuano hiyo itaanza Juni 3 hadi 10 ikishirikisha timu 8 kutoka Tanzania Bana na Visiwani pamoja na wenyeji Kenya. Simba inaondoka bila mshambuliaji wake nyota, Emmanuel Okwi, nahoadha wake John Bocco huku ikijumuisha wachezaji wake wawili wapaya. Marcel Kaheza ambaye amerejea Simba akitoa Majimaji atakuwa mmoja wao, lakini Adam Salamba ataondoka Jumamosi kuungana na Simba. Mmoja wa wakongwe ambaye anarejea katika kiwango chake, Haruna Niyonzima ni kati ya watu waliojumuishwa katika kikosi hicho kitakachoongozwa na Pierre Lechantre. Msafara utaongozwa na mkongwe Hamisi Kisiwa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Said Tuli pamoja Msemaji wake, Haji Sunday Manara. KIKOSI: 1. Aishi Manula 2. Said Mohamed 3. Ally Salim 4. Ally Shomary  5. Paul Bukaba  6. Erasto Nyoni 7. Yusufu Mlipili 8. Mohamed Hussein ...

MARCEL KAHEZA ATUA MSIMBAZI RASIMI

Image
Mshambuliaji aliyekuwa anichezea Majimaji FC, Marcel Kaheza, amethibisha kusaini mkataba wa awali na klabu ya Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini msimu huu. Kaheza ambaye ambaye amehitimisha safari ya kuichezea Majimaji FC iliyoshuka daraja rasmi leo baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Simba, atakuwa na kikosi cha wekundu hao wa Kariakoo katika msimu ujao wa ligi. Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Simba akikuzwa kutoka kikosi B, anakuwa anarejea kwa mara ya pili Msimbazi baada ya kupachika mabao 14 kwenye ligi akiwa na Majimaji msimu huu. Mbali na Kaheza, taarifa zimeeleza pia kuwa Simba imeshanyaka saini ya Mshambuliaji wa Lipuli FC, Sadam Salamba. Baada ya Kaheza aliyekuwa wa kwanza kusaini na Simba, Salamba anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na mabingwa hao mara 19 katika Ligi Kuu Vodacom.

HUU NDO UJUMBE WA MO SALAH ALIOUANDIKA MWENYEWE

Image
Baada ya kuenea kwa taarifa zilizoeleza kuwa nyota wa Liverpool na timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah atakosekana katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia huko Russia, mchezaji huyo amesema atakuweko kwenye mashindano hayo. Salah aliumia sana juzi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool baada ya kuchezewa rafu na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos katika mchezo ambao ulimalizika kwa Madrid kushinda mabao 3-1 na kunyakua ubingwa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter pia Facebook, Salah ameandika kuwa ana imani atakuwepo kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inayotaraji kuanza siku kadhaa zilizosalia.

ADAM SALAMBA ATUA SIMBA RASIMI KWA DAU HILI

Image
Mshambuliaji wa Lipuli FC ya Iringa, Adam Salamba, ana asilimia kubwa ya kuichezea Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, ni baada ya kumalizana na mabingwa hao wapya wa ligi. Simba imefanikisha usajili wa Salamba baada ya kuwazidi ujanja watani wao wa jadi, Yanga wal­iokuwa wanaiwania saini ya mshambuliaji huyo kwa ajili ya kumtumia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga walikuwa wa kwanza kupeleka barua ya Lipuli ya kumuomba mshambuliaji huyo ili wamtumie kwenye mi­chuano hiyo ya kimataifa na kujibiwa kanuni zinawazuia Salamba kutua Yanga kuto­kana na kuzichezea timu mbili katika msimu mmoja, Stand United na Lipuli. Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti la  Championi  limezipata kutoka ndani ya uongozi wa Simba, tayari taratibu zote za usajili wa Salamba zimekamilika na kilichobakia ni msham­buliaji huyo kusaini pekee. Mtoa taarifa huyo alisema, mshambuliaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa kuichezea Simba leo Jumatatu jioni...

MAMILIONI YA DK SHIKA YATUA NCHINI RASIMI HIZI NDIO MIPANGO ZAKE

Image
                             Angalia hapa

HILI NDO DAU LA SALAMBA

Image
Baada ya kuwabania Yanga kuwapatia mshambuliaji wao, Adam Salamba, uongozi wa Lipuli FC umetangaza kiasi cha fedha kwa klabu yoyote inayohitaji kumnyakua mchezaji huyo. Taarifa zinaeleza kuwa Lipuli wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 50 pekee ili kumuachia mchezaji huyo aliyekuwa kwenye fomu nzuri msimu huu. Awali Yanga walituma maombi ya kumuhitaji Salamba kwa ajili ya kuwapiga tafu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini yaligonga mwamba kutokana na kanuni za TFF, CAF na FIFA kutoruhusu mchezaji kucheza zaidi ya timu mbili ndani ya msimu mmoja. Inaelezwa kuwa klabu za Simba na Azam FC ndizo zilizoweka nia ya dhati kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo yanaendelea mpaka sasa. Wakati huo Yanga ambao walihitaji nia ya kuwa naye bado hawajazungumza chochote mpaka sasa kama wana lengo la kumsajili au la.