MKUDE ATAJWA KUWA KIUNGO BORA WA LIGI KUU MSIMU HUU


Soma magazeti ya leo hapa


Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ametajwa kuwa ndiye kiungo bora mkabaji msimu huu kuliko wote.

Hali hiyo inatokana na uwezo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani wakati akiitumikia timu yake hiyo katika Ligi Kuu Bara.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu wamemtaja Mkude kuwa ndiye kiungo bora msimu huu.

Beki wa kati wa Mwadui FC, Idd Mobby amesema Mkude ni bora zaidi kuliko msimu uliopita na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu yake jambo ambalo linamfanya awe vizuri.

Naye beki wa Prisons, Salum Kimenya, amesema: “Simba wanapaswa kujivunia mchezaji huyo, kawafanyia kazi kubwa, ukiangalia mechi nyingi ambazo hajacheza mabeki wao walipata shida sana tofauti na anapokuwepo uwanjani, binafsi naona anastahili kuwa namba sita bora msimu huu.”

Kutoka Championi
SOMA MAGAZETI YA LEO HAPA

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA