SABABU ZA CHIRWA, TSHISHIMBI, NA YONDANI KUTOSAFIRI NA TEAM KWENDA ALGERIA
SOMA MAGAZETI YA LEO MICHEZO HAPA
Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa wachezaji hao waliosalia nchini baada ya kukosekana katika msafara wa kikosi kilichosafiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho kuwa wana matatizo binafsi na si madai ya mishahara.
Inaelezwa kuwa uongozi huo umesema wachezaji hao wameshindwa kutokana na kukabiliwa na changamoto, ambapo imeelezwa Papy Kabamba na Kelvin Yondani waliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba.
Mbali na wachezaji hao kuwa majeruhi, Mzambia Obrey Chirwa naye amesalia kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Malaria hivyo naye amesalia Dar es Salaam ili kuuguza hali yake.
Kumekuwa na taarifa zinazodai kuwa wachezaji hao wameshindwa kusafiri kuelekea Algeri kutokana na mgomo baridi juu ya madai ya stahiki zao ikiwemo mishahara.
Yanga itakuwa inacheza na USM Alger katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shrikisho Afrika, kesho Jumapili kuanzia majira ya saa 4 kamili usiku.
Comments
Post a Comment