UJUMBE WA MAMA KWA WATU WOTE

Katika wimbo wa Lucky Dube "God Bless The Women" anasema:

Katikati ya usiku wa manane, nilisikia sauti nyororo ya mwanamke ikiomba. Ikiomba kwa uchungu. Akiomba kwa ajili ya watoto wake, akiomba kwa ajili ya elimu yao, ikiomba kwa ajili ya kesho yao.
Nilimsikia pia akiomba kwa ajili ya mwanaume aliyemtelekeza.

Akamkimbia na kumuachia watoto, ambao sasa anahangaika mwenyewe kuwalea.

Kila siku tunasifu mashujaa wa aina mbalimbali. Lakini kuna mashujaa tunaowasahau. Wanawake wa dunia hii. Hawa ni mashujaa wa kweli. Mashujaa wasio na tuzo. Hata hali iwe ngumu vp hawakimbii wajibu wao. Husimama na kupambana.

Maisha yanapokuwa magumu sana husimama imara na kuyakabili. Hawatelekezi watoto. Hupambana kwa hali yoyote kuwalinda. (Wako tayari kushinda njaa ili watoto wale, wapo tayari kufa ili watoto waishi). Mwenyezi Mungu atubariki wanawake wote

Share na wengine
Imeandikwa na mwalimu habelnoah

Comments

Popular posts from this blog

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

YANGA YAJIBIWA HIVI NA TFF KUHUSU KUOMBA KUJITOA KAGAME CUP

MASHINDANO MENGINE TOFAUTI NA KAGAME KUANZA 29, JUNE SIMBA NA YANGA NDANI RATIBA NZIMA HII HAPA