HISTORIA YA KABILA LA WAFIPA KUTOKA SUMBAWANGA
WAFAHAMU WAFIPA.. Wafipa ni jamii ya wabantu waishio katika mkoa wa Rukwa. Shughuli kuu za uchumi kwa jamii hii ni kilimo na ufugaji. Baadhi hujishughulisha na uvuvi na uwindaji.na wale wanaoishi pembeni mwa mto Rukwa hujishughulisha na uvuvi kama moja ya shughuli za kiuchumi. Wafipa wana historia ndefu hasa katika teknolojia ya ufuaji wa chuma kuanzia arne ya 17. Kama ilivyo kwa jamii nyingi, mila na desturi za wafipa ni suala linaloheshimiwa. Ndoa hufanywa kwa kufuata taratibu za kimila. Kijana akifikia umri wa kuoa hushauriwa na wazazi wake kuhusu ukoo mzuri wa kutafuta mke. Masuala yanayozingatiwa ni pamoja na kuchapa kazi, kuepuka koo zenye magonjwa na zisizokuwa na uzao. Kijana akishaoa hukaa karibu na wazazi kwa muda wa mwaka mmoja ili kujifunza jinsi ya kuendesha familia baada ya hapo huweza kujenga sehemu nyingine. Wafipa: Kabila lililoamini uwepo wa Mungu wa mbinguni... WAFIPA ndilo kabila kubwa kuliko mengine yaliyopo katika mkoa wa Rukwa. Makabila mengine ni...