Posts

UJUMBE WA MAMA KWA WATU WOTE

Image
Katika wimbo wa Lucky Dube "God Bless The Women" anasema: Katikati ya usiku wa manane, nilisikia sauti nyororo ya mwanamke ikiomba. Ikiomba kwa uchungu. Akiomba kwa ajili ya watoto wake, akiomba kwa ajili ya elimu yao, ikiomba kwa ajili ya kesho yao. Nilimsikia pia akiomba kwa ajili ya mwanaume aliyemtelekeza. Akamkimbia na kumuachia watoto, ambao sasa anahangaika mwenyewe kuwalea. Kila siku tunasifu mashujaa wa aina mbalimbali. Lakini kuna mashujaa tunaowasahau. Wanawake wa dunia hii. Hawa ni mashujaa wa kweli. Mashujaa wasio na tuzo. Hata hali iwe ngumu vp hawakimbii wajibu wao. Husimama na kupambana. Maisha yanapokuwa magumu sana husimama imara na kuyakabili. Hawatelekezi watoto. Hupambana kwa hali yoyote kuwalinda. (Wako tayari kushinda njaa ili watoto wale, wapo tayari kufa ili watoto waishi). Mwenyezi Mungu atubariki wanawake wote Share na wengine Imeandikwa na mwalimu habelnoah

KWA WANA MAKUMIRA WOTE

Image
*_SHUKRANI_ _BAADA YA UCHAGUZI*_  Mimi Gwakisa Mwaipopo &Milembe Vedastus tuliokuwa wagombea wa Urais 2018-2019 wa serikali ya TUMaSO tunapenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kutupa fursa ya kugombea nafasi hii ikiwa ni pamoja na kukamilisha mchakato salama.  Kipekee, tuushukuru uongozi wa chuo, Tume, Serikali ya TUMaSO, na Wabunge wote. Tunashukuru kwa umakini, na uvumilivu wenu.  Aidha, tunapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wana-team wote kwa moyo wa pekee na wa upendo mno. Kwa kweli mm na Milembe hatuna chakuwalipa, Mungu pekee ajua kuwapeni ujira wake.  Tunazidi kuwashukuru mno wanafunzi wenzetu wote wa vitivo vyote kwa kutuunga mkono kwa asilimia 28% ya kura zote. Kwetu tumeona mlivyo-Play your part. Tumeona mlivyo muunga mkono Mhe. Chacha kwa asilimia 32% hakika mmetimiza wajibu wenu wa Kikatiba. Aidha,  tunapenda kuwashukuru mno kwa kumuunga mkono Mhe. Lameck Rais Mteule wa serikali ya TUMaSO kwa kumuunga mkono kwa 38...

MAHAKAMA YA KISUTU YATOA AMRI HANS POPE KUKAMATWA

Image
 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu imetoa amri ya Mwenyekiti wa Kamati ya    Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani hapo kuunganishwa katika kesi    ya utakatishaji fedha inayomkabili rais wa timu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu'. Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha    kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani. Amri hiyo imetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya wakili    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini    (TAKUKURU), Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao. Swai alidai kuwa amewatafuta washitakiwa hao toka machi tatu mwaka huu    bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani

OKWI NA BOKO WAVUNJA NA KUWEKA REKODI AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA

Image
Wakati kikosi cha Simba kikijiandaa kupambana na Yanga, Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, washambuliaji wa timu hiyo, Mganda, Emmanuel Okwi na John Bocco wamewashangaza wapenzi na mashabiki wa timu hiyo. Imebainika kuwa wachezaji hao wawili wamefanikiwa kuandika rekodi ya pekee ndani ya klabu hiyo ambayo haijawahi kuandikwa na washambuliaji wengine waliowahi kuitumikia timu hiyo kwa zaidi ya miaka sita. Rekodi hiyo ambayo wameiweka wachezaji hao ni ya kufunga mabao mengi mpaka sasa kushinda pacha za washambuliaji wengine waliowahi kuitumikia timu hiyo katika miaka sita iliyopita. Okwi na Bocco wameifungia Simba mabao 33 kati 58 ambayo timu hiyo imeshafunga kwenye ligi kuu msimu huu huku ikiwa na mechi tano mkononi ili kumaliza ligi hiyo. Msimu wa 2011/12, safu ya ushambuliaji ya Simba ilikuwa ikiundwa na Okwi na Mzambia, Felix Sunzu ambapo mpaka mwisho wa msimu walifunga mbao 19 kati 47. Okwi alifunga mabao 12 huku Sunzu akifunga mabao 7. Msimu wa 2012/13, safu ya u...

KICHUYA NA MSUVA WAONGELEWA BUNGENI LEO SIKIA YALIYO ZUNGUMZWA

Image
jana katika Makao Makuu ya Bunge jijini Dodoma kwa hoja mbalimbali kuendelea kujadiliwa zinahusiana na masuala ya nchi. Wakati kikao kikielekea mwishoni, Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Wilaya ya Ilala, Mussa Azzan Zungu, aliwamchokea swali la kiaina Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harisson Mwakyembe, kuhusiana na kufungiwa kwa wimbo wa Mwanaume Mashine ulioimbwa na Msanii, Msaga Sumu. Zungu alimuuliza Mwakyembe kwanini ameufungia wimbo huo wakati umewataja wachezaji Simon Msuva (aliyekuwa anaichezea Yanga) na Shiza Kichuya ilihali timu hizo zinakutana kesho kwenye Uwanja wa Taifa. Zungu aliwataja wachezaji hao kutoka na namna mchezo huu wa watani wa jadi jinsi unavyovuta hisia za mashabiki na wadau wengi wa soka nchini ambazo zitakuwa zinavaana Jumapili hii ya Aprili 29 2018. Swali hilo lilipelekea kuwaacha hoi wabunge wengi ambao walianguka kwa kicheki na ndipo Mh. Zungu akafunga kikao na kuwataka wabunge watakutana wakati mwingine kuendelea na vikao

KOCHA WA AZAM FC AFUNGIWA MECHI HIZI KWA KOSA LA KUMTUKANA REFA NA KUAMBIWA HIVI

Image
MZUNGU WA AZAM ASIMAMISHWA LIGI KUU KWA KUMTUSI REFA Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA Mromania wa Azam FC, Aristica Cioba amesimamishwa hadi suala lake la kumtukuna Mwamuzi baada ya mechi kumalizika litakaposikilishwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi kutokana na makosa anayodaiwa kuyafanya katika mechi namba 194 dhidi ya Njombe Mji. Kabla ya kumtukana Mwamuzi, Kocha huyo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) kwa kupinga maamuzi kwa maneno na vitendo katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 15, 2018 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

KOCHA MKONGOMANI WA YANGA ANYANG'ANYWA JEZI YENYE LANGI YA SIMBA AAMBIWA HIVI

Image
Baada ya kuwasili jana mjini Morogoro na kupata nafasi ya kukinoa kikosi cha Yanga kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, jezi ya Kocha Mkongomani Mwinyi Zahera yawa gumzo kwa baadhi ya mashabiki wa timu zote mbili. Zahera alitinga Uwanjani kuishuhudia timu yake mpya akiwa amevalia uzi mweusi wenye micharazo ya rangi nyekundu kwenye mabega, rangi ambayo haijawahi kutumika kabisa katika klabu hiyo yenye maskani yake katika mitaa ya Twiga, iliyo Jangwani, Kariakoo. Baadhi ya mashabiki ikiwemo wale wa Yanga na Simba, wamekuwa wakihoji imekuwa avae rangi ambazo hazitumiki ndani ya klabu. Wapo wale walioandika mitandaoni haswa wa upande wa pili wakitupa vijembe kuwa Mkongo huyo ana damu ya Simba kutokana na rangi hiyo nyekundu. Rangi ya Yanga ambayo inatambulika siku zote ni kijani na njano, pia hivi karibuni wamekuwa wakitumia nyeusi haswa katika mechi za ugenini. Kitendo cha Zahera kuvaa rangi hiyo ambayo hutumiwa na watani zao wa jadi Simba, imekuwa gumzo kubwa zaidi kwa baadhi ya mashabiki...