Posts

Showing posts from May, 2018

YANGA YASAFIRI NA HAWA TU , WENGINE WOTE WABAKI NCHINI

Image
Kikosi cha Yanga kimeondoka asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup inayoanza kesho jijini Nairobi. Jumla ya wachezaji  20 walioondoka ni Makipa Youthe Rostand na Ramadhani Kabwili, Mabeki ni Hassani Kessy, Haji Mwinyi, Abdalah Shaibu Ninja, Pato Ngon yani na Said Juma Makapu. Viungo ni Papy Tshishimbi, Raphael Daudi, Thaban Kamusoko, Maka Edward, Said Mussa Bakari, Baruani Akilimali, Pius Buswita na Yusuph Mhilu. Washambuliaji ni Ibrahim Ajibu, Yohana Mkomola, Matheo Anthony, Juma Mahadhi na Amis Tambwe. Yanga wataanza kibarua chao dhidi ya Kakamega Home Boys Jumapili ya June 03 2018 huku Kocha wake, Mwinyi Zahera aikielezwa ataungana na kikosi chake nchini humo. Waliobaki nchini ni Juma Abdul, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Andrew Vicent Dante, Gadiel Michael, Geofrey Mwashiuya Emmanuel Martin, Nadir Haroub Canavaro na Benno Kakolanya.

SIMBA YASAFIRI NA WACHEZAJI HAWA PAMOJA NA WALE WAPYA WOTE

Image
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba walitarajiwa kuondoka leo na kikosi cha watu 25 kwenda nchini Kenya ambao itafanyika michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup. Michuano hiyo itaanza Juni 3 hadi 10 ikishirikisha timu 8 kutoka Tanzania Bana na Visiwani pamoja na wenyeji Kenya. Simba inaondoka bila mshambuliaji wake nyota, Emmanuel Okwi, nahoadha wake John Bocco huku ikijumuisha wachezaji wake wawili wapaya. Marcel Kaheza ambaye amerejea Simba akitoa Majimaji atakuwa mmoja wao, lakini Adam Salamba ataondoka Jumamosi kuungana na Simba. Mmoja wa wakongwe ambaye anarejea katika kiwango chake, Haruna Niyonzima ni kati ya watu waliojumuishwa katika kikosi hicho kitakachoongozwa na Pierre Lechantre. Msafara utaongozwa na mkongwe Hamisi Kisiwa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Said Tuli pamoja Msemaji wake, Haji Sunday Manara. KIKOSI: 1. Aishi Manula 2. Said Mohamed 3. Ally Salim 4. Ally Shomary  5. Paul Bukaba  6. Erasto Nyoni 7. Yusufu Mlipili 8. Mohamed Hussein ...

MARCEL KAHEZA ATUA MSIMBAZI RASIMI

Image
Mshambuliaji aliyekuwa anichezea Majimaji FC, Marcel Kaheza, amethibisha kusaini mkataba wa awali na klabu ya Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini msimu huu. Kaheza ambaye ambaye amehitimisha safari ya kuichezea Majimaji FC iliyoshuka daraja rasmi leo baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Simba, atakuwa na kikosi cha wekundu hao wa Kariakoo katika msimu ujao wa ligi. Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuichezea Simba akikuzwa kutoka kikosi B, anakuwa anarejea kwa mara ya pili Msimbazi baada ya kupachika mabao 14 kwenye ligi akiwa na Majimaji msimu huu. Mbali na Kaheza, taarifa zimeeleza pia kuwa Simba imeshanyaka saini ya Mshambuliaji wa Lipuli FC, Sadam Salamba. Baada ya Kaheza aliyekuwa wa kwanza kusaini na Simba, Salamba anakuwa mchezaji wa pili kujiunga na mabingwa hao mara 19 katika Ligi Kuu Vodacom.

HUU NDO UJUMBE WA MO SALAH ALIOUANDIKA MWENYEWE

Image
Baada ya kuenea kwa taarifa zilizoeleza kuwa nyota wa Liverpool na timu ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah atakosekana katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia huko Russia, mchezaji huyo amesema atakuweko kwenye mashindano hayo. Salah aliumia sana juzi katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool baada ya kuchezewa rafu na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos katika mchezo ambao ulimalizika kwa Madrid kushinda mabao 3-1 na kunyakua ubingwa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter pia Facebook, Salah ameandika kuwa ana imani atakuwepo kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi inayotaraji kuanza siku kadhaa zilizosalia.

ADAM SALAMBA ATUA SIMBA RASIMI KWA DAU HILI

Image
Mshambuliaji wa Lipuli FC ya Iringa, Adam Salamba, ana asilimia kubwa ya kuichezea Simba kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, ni baada ya kumalizana na mabingwa hao wapya wa ligi. Simba imefanikisha usajili wa Salamba baada ya kuwazidi ujanja watani wao wa jadi, Yanga wal­iokuwa wanaiwania saini ya mshambuliaji huyo kwa ajili ya kumtumia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga walikuwa wa kwanza kupeleka barua ya Lipuli ya kumuomba mshambuliaji huyo ili wamtumie kwenye mi­chuano hiyo ya kimataifa na kujibiwa kanuni zinawazuia Salamba kutua Yanga kuto­kana na kuzichezea timu mbili katika msimu mmoja, Stand United na Lipuli. Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti la  Championi  limezipata kutoka ndani ya uongozi wa Simba, tayari taratibu zote za usajili wa Salamba zimekamilika na kilichobakia ni msham­buliaji huyo kusaini pekee. Mtoa taarifa huyo alisema, mshambuliaji huyo anatarajiwa kusaini mkataba wa kuichezea Simba leo Jumatatu jioni...

MAMILIONI YA DK SHIKA YATUA NCHINI RASIMI HIZI NDIO MIPANGO ZAKE

Image
                             Angalia hapa

HILI NDO DAU LA SALAMBA

Image
Baada ya kuwabania Yanga kuwapatia mshambuliaji wao, Adam Salamba, uongozi wa Lipuli FC umetangaza kiasi cha fedha kwa klabu yoyote inayohitaji kumnyakua mchezaji huyo. Taarifa zinaeleza kuwa Lipuli wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 50 pekee ili kumuachia mchezaji huyo aliyekuwa kwenye fomu nzuri msimu huu. Awali Yanga walituma maombi ya kumuhitaji Salamba kwa ajili ya kuwapiga tafu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini yaligonga mwamba kutokana na kanuni za TFF, CAF na FIFA kutoruhusu mchezaji kucheza zaidi ya timu mbili ndani ya msimu mmoja. Inaelezwa kuwa klabu za Simba na Azam FC ndizo zilizoweka nia ya dhati kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo yanaendelea mpaka sasa. Wakati huo Yanga ambao walihitaji nia ya kuwa naye bado hawajazungumza chochote mpaka sasa kama wana lengo la kumsajili au la.

YAMOTO BAND WIMBO MPYA BARUA dowbload

Image
.                                             CLICK HERE

SPORTS PESA YAIZAWADIA SIMBA SC KWA KUTWAA UBINGWA

Image
SPORTS PESA YAIZAWADIA SIMBA SC Wadhamini wakuu wa Club yetu ya Simba wameizawadia Shilingi Million 100 Simba Sc kama Zawadi ya Ubingwa Wa VPL pesa hiyo imetokewa Leo hii majira ya asubuhi

MENEJA WA DIAMOND ATIWA MBARONI KISA DENI LA MILIONI 250

Image
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa Msanii Diamond Platnumz,  Hamis Taletale ‘Babu Tale’, ametiwa  mbaroni na kufikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es  Salaam. Babu Tale amekamatwa kufuatia amri iliyotolewa Februari 16, 2018 na Naibu Msajili wa Mahakama  Kuu Kanda Maalum, Wilbard Mashauri iliyoelekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale. Amri hiyo pia, ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine. Hata hivyo, Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama hiyo ikatoa amri nyingine kama hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa wakitafutwa bila mafanikio hadi jana alipokamatwa. Mahakama hiyo iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh250 milioni, baada y...

TANZANIA YA TIKISA KOMBE LA DUNIA RUSSIA

Image
Na  Mohamed Mansour Nassor, RUSSIA Mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto yameendelea tena leo mjini Moscow nchini Urusi katika uwanja wa klabu ya Lokomotive Moscow ambapo michezo ya nusu fainali ilichezwa ambapo Tanzania ilipambana na Uingereza na mwisho wa mchezo Tanzania imefanikiwa kutinga fainali kwa kishindo kwa kuibamiza na kuisambaratisha bila ya huruma timu ya Uingereza kwa magoli 2-1. Mabao ya Tanzania yalifungwa na mlinzi Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari. Tanzania itacheza fainali na Brazil kesho kutwa ambapo Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali goli 1-0.  Magoli ya mechi zote yalifungwa kipindi cha pili huku Tanzania wakiumiliki mchezo kwa asilimia kubwa sana na watoto wa kitanzania walionyesha umahiri mkubwa sana mbele ya Mheshimiwa Balozi wetu na wa Tanzania nchini Urusi na pia maafisa wa Ubalozi wetu walihudhuria kutazama mechi hio.  Kwa upande mwengine John Wroe ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa wa Shirika la Street Child...

LULU AACHIWA RASIMI

Image
Dar es Salaam.  Mcheza filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu amebadilishwa kifungo na sasa atatumikia adhabu hiyo akiwa nje yaani ‘kifungo cha nje’. Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Akizungumza na MCL Digital Jumatatu Mei 14, 2018, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu  na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam. “Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje

HATIMAYE TSHISHIMBI AREJEA KWAO CONGO

Image
Akijiuguza kwa muda wa wiki mbili bila matarajio ya kupona, kiungo mkabaji wa Yanga Mkongoman, Papy Kabamba Tshishimbi ameamua kurudi kwao fasta kwa ajili ya kwenda kujitibia kwa miti shamba. Kiungo huyo yupo nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili akiuguza majeraha yake ya enka aliyoyapata katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika walipokutana na Wollayta Dicha ya Ethiopia na hata kwenye mchezo dhidi ya Rayon Jumatano, hatakuwepo. Staa huyo aliyewabamba mashabiki wa Yanga, hadi sasa amekosa mechi mbili dhidi ya USM Algier’s na ile ya Prisons na hata ya leo Jumapili na Mtibwa mjini Morogoro ataikosa. Habari za ndani zinasema kwamba amerudi kwao baada ya kutoridhishwa na matibabu aliyokuwa akipata hapa nchini na amewaambia viongozi kuwa kuna sehemu kule kwao anaweza kupata dawa za kienyeji zikamrudisha kwenye hali nzuri. Kocha wa Yanga, Zahera Mwinyi alipoulizwa kuhusu mchezaji huyo alisema; “Ni kweli Tshishimbi hayupo na timu ana majeraha ya enka aliyoyapata katika me...

RAIS MAGUFULI AISAIDIA SIMBA KUWEKA HISTORIA HII DODOMA

Image
Kikosi cha Simba kimeondoka jana jijini Dar es Salaam kuelekea Singida kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United. Simba ambao tayari ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameondoka wakiwa na rekodi ya kuutwaa ubingwa wa ligi bila kupoteza mchezo hata mmoja huku wakiwa na mechi tatu mkononi. Kikosi hicho kilipitia Dodoma na kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kuendelea na safari ya Singida kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa Mei 12 2018. Simba wameandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuweka kambi ya muda mfupi Dodoma baada ya kupewa hadhi ya kuwa Jiji na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Joseph Magufuli siku kadhaa zilizopita. Rais Magufuli alitangaza rasmi Dodoma kuwa jiji katika siku ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika Aprili 26 2018. Kitendo cha Simba kupita Dodoma na kuweka kambi fupi jana kimeipa historia ya kuwa klabu ya kwanza inayoshiriki Ligi Kuu Bara kufanya hivyo ndani ya jiji hilo jip...

TENGENEZA PESA KWA KUTUMIA MBs TU BILA YA MASHARTI YOYOTE

Image
                                                                  BOFYA HAPA FUATA MAELEKEZO HAPO CHINI UKISHINDWA NIFATE INBOX KWA 0752579739 Tengeneza pesa ukiwa na MB tu kwa kubofya hapo chini utafuata maelekezo utafungua account kwa kuingia sehemu iliyo andikwa registration upande wako wa kushoto utatengeneza user name na password unayoipenda wewe mwenyewe baada ya kutengeneza account yako bofya sehemu iliyo andikwa START WATCHING PAYED ADS baada ya hapo utaletewa namba 4 utajaza sehemu inayo stahili hivo hivi itakuwa mwendelezo wa kujaza namba nne kadri unavyo jaza ndivyo hivyo unavyolipwa ukitazama upande wa kushoto chini ya user name yako kuna sehem imeandikwa EARNS sasa kadri unavyo zidi kujaza hzo namba ndvyo hivyo hlyo sehem inazid kuongeza earns kutoa pesa yako mpaka utimize dollar 150 kisha utabofya sehem...

AJIBU AJAALIWA KUPATA MTOTO WA KIKE AANDIKA HAYA KWA UCHUNGU

Image
Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuwa familia ya Mshambuliaji wake, Ibrahim Ajibu, imejaaliwa kupata mtoto wa kike. Ajibu alishindwa kusafiri na kikosi cha Yanga kuelekea Algiers, Algeria kwa ajili ya mechi ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger. Mchezaji huyo amesema kuwa ujauzito wa mkewe umepitia changamoto mbalimbali, jambo lililopelekea hofu kubwa kwake lakini ameeleza kumshukuru Mungu kwa kufanikiwa kujifungua salama. Mbali na mkewe kupata mtoto, Ajibu amesema kuwa ameumizwa na baadhi ya mashabiki waliomtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu wakimuandama kuwa hajasafiri na timu. "Nashukuru Mungu ametujaalia kupata mtoto wa kike, hapo kabla nilikuwa na hofu kubwa kwasababu ujauzito wa mke wangu ulikuwa na matatizo makubwa, kuna wakati nilikuwa nina hofu juu ya maisha yake. "Naumizwa na wanaonishambulia kupitia sms kuwa nimegoma kuichezea timu, sina sababu ya kufanya hivyo maana mpira ni kazi yangu" amesem...

MKUDE ATAJWA KUWA KIUNGO BORA WA LIGI KUU MSIMU HUU

Image
Soma magazeti ya leo hapa Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ametajwa kuwa ndiye kiungo bora mkabaji msimu huu kuliko wote. Hali hiyo inatokana na uwezo wake mkubwa ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani wakati akiitumikia timu yake hiyo katika Ligi Kuu Bara. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali za ligi kuu wamemtaja Mkude kuwa ndiye kiungo bora msimu huu. Beki wa kati wa Mwadui FC, Idd Mobby amesema Mkude ni bora zaidi kuliko msimu uliopita na amekuwa na msaada mkubwa kwa timu yake jambo ambalo linamfanya awe vizuri. Naye beki wa Prisons, Salum Kimenya, amesema: “Simba wanapaswa kujivunia mchezaji huyo, kawafanyia kazi kubwa, ukiangalia mechi nyingi ambazo hajacheza mabeki wao walipata shida sana tofauti na anapokuwepo uwanjani, binafsi naona anastahili kuwa namba sita bora msimu huu.” Kutoka Championi SOMA MAGAZETI YA LEO HAPA

Usipitwe na uhondo wa Magazeti ya jumamosi ya taree 5.2018

Image

SABABU ZA CHIRWA, TSHISHIMBI, NA YONDANI KUTOSAFIRI NA TEAM KWENDA ALGERIA

Image
SOMA MAGAZETI YA LEO MICHEZO HAPA Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa wachezaji hao waliosalia nchini baada ya kukosekana katika msafara wa kikosi kilichosafiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho kuwa wana matatizo binafsi na si madai ya mishahara. Inaelezwa kuwa uongozi huo umesema wachezaji hao wameshindwa kutokana na kukabiliwa na changamoto, ambapo imeelezwa Papy Kabamba na Kelvin Yondani waliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba. Mbali na wachezaji hao kuwa majeruhi, Mzambia Obrey Chirwa naye amesalia kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Malaria hivyo naye amesalia Dar es Salaam ili kuuguza hali yake. Kumekuwa na taarifa zinazodai kuwa wachezaji hao wameshindwa kusafiri kuelekea Algeri kutokana na mgomo baridi juu ya madai ya stahiki zao ikiwemo mishahara. Yanga itakuwa inacheza na USM Alger katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shrikisho Afrika, kesho Jumapili kuanzia majira ya saa 4 kamili usiku.

CHIRWA NA YONDANI WAIGOMEA YANGA

Image
Mkataba wa beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani na ule wa Obrey Chirwa inamalizika mwishoni mwa msimu na wachezaji hao wamegomea mazungumzo ya mikataba mipya. Yondani amekuwa mhimili wa  safu  ya ulinzi ya Yanga msimu huu huku Chirwa akiwa kinara wa mabao, ameifunga Yanga mabao 12 kwenye ligi. Inaelezwa wawili hao wamegomea mazungumzo ya mikataba mipya hivyo wanaweza kuondoka wakiwa wachezaji huru mwisho wa mwezi huu msimu utakapomalizika kama jitihada zaidi za kuwabakisha hazitafanyika. Kuna taarifa klabu ya ZESCO United ambayo sasa inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga George Lwandamina inawanyemelea wachezaji hao. Chirwa pia amekuwa akihusishwa na klabu ya Simba japo mwenye mara kadhaa amekanusha juu ya uwezekano wa kutimkia kwa wapinzani hao wa Yanga. Yondani na Chirwa ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakusafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda nchini Algeria kuikabili USM Alger kwenye mchezo wa kwanza wa kundi D kombe la shirikisho barani Afrika.

Uongozi wa Simba waitisha Mkutano wa dharura

Image
 Uongozi wa Simba waitisha Mkutano wa dharura Klabu ya Simba kupitia kwa kaimu mwenyekiti Salim Abdallah “Try Again” Imeitisha Mkutano wa Dharura kuhusiana na mabadiliko ya katiba Jumapili 20.5.2018 Barua Hii hapa chini

YONDANI ASIMAMISHWA KUITUMIKIA YANGA KWA MDA USIO JULIKANA

Image
Bodi ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi. Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa. Tazama mechi live atretical vs arsenal "Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake," alisema Wambura. Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0. Suala hilo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau, wakiwemo waliomtetea Yondani na walioona haikuwa sahihi

Download wimbo mpya HARMONIZE FT SARKODIE dm chick

Image
                                              >>>>> bofya hapa<<<<