TSHISHIMBI KUTOKA YANGA KWENDA SIMBA AZUNGUMZA HAYA
Kiungo Papy Tshishimbi ameondoka nchini na kurejea kwao DR Congo kwa ajili ya mapumziko. Tshishimbi amekuwa akihusishwa na kujiunga na Simba, jambo ambalo limewapa hofu na hasira baadhi ya mashabiki wa Yanga. Tshishimbi hakuwa amewahi kulizungumzia suala hilo lakini jana amekutana na Salejembe jijini Nairobi, Kenya na kuweka wazi kila kitu. Tshishimbi amesema anareja kwao kwa mapumziko akiwa bado ni mchezaji wa Yanga na atarejea baada ya mapumziko. Kuhusiana na suala la Simba, hii ndiyo kauli yake. “Kuhusu Simba ninasikia tu kwa kweli. Lakini hakuna ambaye amewahi kunifuata tukalizungumzia suala hilo.” Alipoulizwa kama Simba wakimfuata, yuko tayari kujiunga nao? “Soka ni biashara rafiki yangu, unajituma na kufanya vizuri ili upae kibiashara na kujiendeleza zaidi. Timu ikifanikiwa, soko linakuwa juu. “Kama Simba wananihitaji, niko tayari wanaweza kusema wanahitaji nini nami niangalie.”